Kenya-Mpango wa serikali wa Shilingi bilioni 20 kukuza utengenezaji wa ndani

(CRI Online) Juni 11, 2021

Serikali ya Kenya imeweka matumaini yake katika maeneo maalum ya uchumi (SEZs) ili kukuza ukuaji wa viwanda katika kaunti katika hatua ambayo inaweza kusaidia sekta ya utengenezaji kupona kutoka mwaka mgumu wa kazi.

Kulingana na Bajeti ya 2021-22 iliyowasilishwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri la Hazina ya Kitaifa Ukur Yatani jana, serikali ya Kenya imetenga Sh20.5 bilioni kwa ajili ya kukuza viwanda vya ndani kupitia wizara anuwai.

Hii ni pamoja na Sh8.3 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya eneo maalum la uchumi la Dongo Kundu SEZ, Sh1.4 bilioni kwa Mradi wa Viwanda na Ujasiriamali wa Kenya na Sh448 milioni kwa Maabara ya Utafiti wa Viwanda ya Kenya.

Hifadhi ya Viwanda ya Naivasha, eneo maalum la uchumi na Miwani,lililoko mjini Kisumu, Hifadhi ya viwanda vya nguo ya Naivasha na Kitovu cha Nguo cha Athi River pia zimepokea mgao wa fedha hizo ili kuziga jeki ukuaji wa viwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha