Tanzania: Serikali Yahimiza Uwekezaji Kilimo mbegu za mafuta

(CRI Online) Juni 15, 2021

Serikali imefungua milango kwa wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo kutoka nchi za Ulaya, kuwekeza nchini Zanzibar katika sekta ya kilimo cha alizeti, ufuta na mbogamboga. Hii inajiri baada ya wawekezaji hawa kuhakikishiwa kuwa kuna ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo na kuanzisha kiwanda cha kuchakata mazao.

Akizungumzana vyombo vya habari jijini Arusha mwishoni mwa wiki, Waziri wa Kilimo na Mifugo, Prof. Aldof Mkenda wakati wa mkutano na wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo kutoka nchi za ulaya, ulioandaliwa na umoja wa wafanyibiashara wa Ulaya nchini Tanzania.

Alisema wawekezaji hao watapunguza changamoto ya mafuta ya kula Pamoja na uzalishaji wa mbegu, kilimo cha matunda na mbogamboga nchini Tanzania ili waje kuwekeza na kuwasaidia wakulima wa Tanzania kupata soko la mazao hayo humo nchini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha