Lugha Nyingine
Benki za maendeleo za mataifa tajiri kuwekeza $80 bilioni Afrika
Benki kubwa za maendeleo za mataifa tajiri duniani Jumatatu zimeahidi kuwekeza dola billioni 80 kwenye makampuni ya Afrika na miradi katika miaka mitano ijayo.
Shirika la kimataifa la fedha (IMF) lilikadiri kuwa nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara zitahitaji msaada wa ziada wa billioni 425 kati ya hivi sasa na 2025.
Msaada huo utatumika kupambana na janga la COVID-19 na kupunguza viwango vya umaskini vilivyoongezeka kutokana na janga hilo.
Kanda hiyo imetaabika sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na ni kwa mara ya kwanza taasisi za maendeleo kutoka Marekani, Ulaya na nchi nyingine tajiri za kundi la G7 kutoa ahadi ya pamoja ya dola billioni 80 kwa bara la Afrika.
David Marshik, afisa mkuu kwenye taasisi ya Marekani inayohusika na ufadhili wa maendeleo ya kimataifa, anasema kuwekeza zaidi barani Afrika hivi sasa ni kipaumbele chini ya utawala wa Rais Biden.
Aina nane maarufu zaidi za maua ya Yunnan hakika kuna moja inayokushangaza zaidi
Korongo wacheza kwenye uwangja wa juu hali ya viumbe yaendelea vizuri mkoani Tibet
Rasilimali ya utamaduni yasukuma mbele ujenzi wa kijiji cha kupendeza cha Luquan mjini Shijiazhuang
Mji wa Zhengzhou warudia katika hali ya kawaida ya uzalishaji na maisha
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma