China yarusha chombo kilichobeba wanaanga kwenda kituo chake kwenye anga ya juu

(CRI Online) Juni 18, 2021

China jana Alhamis imerusha chombo cha Shenzhou -12 kilichobeba wanaanga watatu, ambacho kinatarajiwa kuwapeleka kwenye kituo chake cha anga ya juu cha Tiangong kwa kazi ya miezi mitatu.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China, chombo hicho kilichobebwa na roketi ya Long March-2F, kilirushwa kwenye kituo cha kurushia cha Jiuquan, kilichopo kwenye jangwa la Gobi kaskazini magharibi mwa China. Hii ni mara ya saba ya chombo cha safari kwenye anga ya juu cha China kupeleka wanaanga kwenye anga ya juu, na ni safari ya kwanza baada ya kipindi cha ujenzi wa kituo kwenye anga ya juu cha China. Pia ni safari ya kwanza baada ya miaka mitano iliyopita tangu safari ya mwisho ya chombo cha safari kwenye anga ya juu cha China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha