Nchi 15 za Afrika Magharibi Zatazamiwa Kutumia Fedha za pamoja Mwaka 2027

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2021

Tarehe 19, viongozi wa nchi za Umoja wa Uchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS) wamedhihirisha huko Accra, mji mkuu wa Ghana, kuwa nchi hizi za umoja huo zitatoa fedha mpya za pamoja “Eco” mwaka 2027. Kuanzia mwaka 2022 hadi mwaka 2026, nchi wanachama za Umoja wa Uchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS) zitatekeleza makubaliano kuhusu kutumia fedha mpya za pamoja.

Umoja wa Uchumi wa Afrika Magharibi uliamua kutoa fedha za pamoja mwaka 2020, lakini kutokana na athari ya Covid-19, ziliahirisha kutekeleza. Hivi sasa Umoja wa Uchumi wa Afrika Magharibi una nchi wanachama 15, na idadi ya watu milioni 385, ambayo inachukua karibu 1/3 ya idadi ya jumla ya watu wa Afrika. Huu ni umoja mkubwa zaidi wa uchumi katika Afrika Magharibi. Hivi sasa nchi wanachama wanane wa umoja huo zinatumia fedha za pamoja, yaani faranga ya Afrika Magharibi ambayo thamani yake inafanana na fedha za euro.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha