Feng Fei: Hatutaruhusu Bandari ya Biashara Huria ya Hainan iwe “Mahali pa Kukwepa Ushuru”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2021

(Picha inatoka tovuti ya China Daily)

Habari za Juni 21 kwenye tovuti ya Xinhua zilisema, serikali ya Mkoa wa Hainan itazuia na kudhibiti kwa nguvu zote hatari ya magendo ya bidhaa bila kutozwa ushuru, na haitaruhusu bandari ya biashara huria ya Hainan iwe "mahali pa kukwepa ushuru".

Tarahe 21, kwenye mkutano wa Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China kuhusu hali husika ya sheria ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, Mkuu wa serikali ya mkoa wa Hainan amesema, ili kuzuia na kudhibiti hatari ya kutorokea utozaji wa uhuru, mkoa wa Hainan umeitisha mkutano kwa mara sita wa kamati ya kazi ya bandari ya biashara huria ya Kamati ya Chama ya Mkoa wa Hainan, ambapo umesikiliza ripoti kuhusu hali ya kuzuia na kudhibiti hatari, na kuunda vikundi 15 vya kazi maalumu ya kuzuia na kudhibiti hatari chini ya uongozi wa Kamati ya Chama ya Mkoa. Kwenye mikutano hiyo, wahudhuria walichambua na kubainisha hatari za aina mbalimbali, kurekebisha kazi zinazohusika, na kuanzisha mfumo kamili wa kutoa tahadhari na kuzuia hatari. Mpaka sasa, hatari kubwa bado hazijatokea kote mkoani au kwenye mfumo husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha