Kituo cha Maonyesho cha Kitaifa (Tianjin) chaanza Maonyesho yake ya Kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2021

(Picha inatoka tovuti ya Xinhua)

Tarehe Juni 24, watazamaji wametembelea maonesho yanayofanyika kwenye ukumbi wa Kampuni ya Tatu ya Ujenzi ya China katika eneo la ujenzi wa mradi wa kwanza la Kituo cha Maonyesho cha Kitaifa (Tianjin).

Siku hiyo, Kituo cha Maonyesho cha Kitaifa (Tianjin) kilifanya maonyesho yake ya kwanza -- Mkutano wa sayansi ya ujenzi wa China, na Maonyesho ya majengo ya teknolojia ya akili bandia bila uchafuzi. Maonyesho hayo yaliendelea hadi Juni 27.

Maonyesho hayo yakifuata kauli mbiu ya "majengo yasiyochafua mazingira yachangia maisha mazuri ya pamoja", "majengo yasiyochafua mazingira yachangia kurekebisha na kudhibiti utoaji wa kaboni", yaitisha Mkutano wa Sayansi ya Ujenzi wa China na Mabaraza zaidi ya 150 sambamba, ambapo wahudhuria walijadili kuhusu njia ya sekta ya ujenzi kujiendeleza kwa sifa bora ya hali ya juu bila uchafuzi mwingi kwa mazingira.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha