Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Brazil unaendelea kuimarika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2021

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Uchumi ya Brazil zimeonesha kuwa, mwezi Mei mwaka huu, urari wa biashara ya nchi ya nje ya Brazil imefikia dola za kimarekani bilioni 9.291 ambayo imeongezeka kwa asilimia 29.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Kati yake uuzaji kutoka Brazili kwenda China umeongezeka usiofuata hali ya kawaida ambayo China inaendelea kuwa nchi kubwa ya kwanza kwa Brazil kusafirisha bidhaa nje. Waziri wa uchumi wa Brazil Bw.Paulo Guedes alisema, maendeleo mazuri ya biashara kati ya China na Brazil yanafanya kazi muhimu kwa uchumi wa Brazil.

Kilimo ni nguzo kuu ya uchumi wa Brazil. Kutokana na mahitaji makubwa ya China juu ya soya na pamba, uuzaji wa nje ya nchi wa bidhaa za kilimo za Brazil ya mwezi Mei uliongezeka kwa asilimia 33.7 kuliko ule wa mwaka jana na kufikia dola ya kimarekani bilioni 13.94 ambayo imekuwa rekodi mpya. Takwimu za Shirikisho la Wakulima wa Pamba zinaonesha kuwa mwezi Mei, mwaka huu uuzaji wa nje ya nchi wa pamba wa Brazil umezidi tani laki 1.15 ambao umekuwa rekodi mpya ya mwezi. Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw. Julio César Busato alisema, uuzaji wa pamba kwa China umechukua karibu asilimia 31 katika uuzaji wa jumla wa Brazil wa mwaka 2020-2021.

“China ni mwenzi mkubwa zaidi wa Brazil katika biashara, pia ni moja ya nchi zinazotoa uwekezaji mkubwa kabisa kwa Brazil.”Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Bw. Carlos Fran a alisema,”Tuna nia thabiti kwa maendeleo ya uhusiano kati ya Brazil na China.”

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha