Maelezo ya kwanza ya picha za katuni kuhusu haki za binadamu za kimarekani
Kuchokoza vita haramu kuvurugisha utaratibu wa dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2021
Maelezo ya kwanza ya picha za katuni kuhusu haki za binadamu za kimarekani
Kuchokoza vita haramu kuvurugisha utaratibu wa dunia
Mchoraji wa picha: Lu Lingxing

Marekani ni nchi inayopenda kabisa kuanzisha vita duniani.

Tangu Marekani ilipotangaza uhuru wake mwaka 1776, katika historia yake ya zaidi ya miaka 240, muda ambao wa kutoshiriki kwenye vita kwa Marekani ni chini ya miaka 20 tu. Kwa mujibu wa takwimu zisizokamilika, kuanzia mwaka 1945 wa kumalizika kwa vita vya pili vya dunia hadi mwaka 2001, kulitokea migorogoro ya kijeshi kwa mara 248 katika maeneo 153 duniani. Kati yake migorogoro iliyoanzishwa na Marekani ilifikia 201 ambayo ilichukua 81% hivi.

Katika vita hivyo Marekani ilivyoshiriki, baadhi yao ni mashambulizi ya kijeshi yaliyoanzishwa kwa kupitia “njia halali” ya kupewa haki na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulioendeshwa na Marekani lakini vingi vyake ni “vita haramu” vilivyochokozwa na Marekani kwa kunyanyua bendera ya “haki ya binadamu”.

Baada ya vita baridi, Marekani ilitumia nguvu zaidi ya kijeshi katika Mashariki ya Kati. Katika hali ambayo ilikuwa haijapewa haki na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hasa haijakubaliwa na Bunge la taifa la Marekani, serikali ya Marekani ilianzisha na kushiriki kwenye vita vya Afghanistan, Iraq, Libya, na Syria. Vita hivyo si kama tu vilisababisha vifo vya watu wengi wasiohesabika, bali pia vilisababisha raia wengi sana kujeruhiwa, na kusababisha hasara kubwa kabisa za mali ambapo mamilioni ya watu walipoteza makazi yao na wamekuwa wakimbizi duniani, haki zao za kuishi, na kujiendeleza zimedhuriwa vibaya, maeneo hayo ya migogoro yamekumbwa na balaa kubwa ya ubinadamu.

Ukweli wa mambo umeonesha kuwa, Marekani inayojidai kubeba "majukumu inayokabidhiwa na Mungu" ndiyo mhalifu mkuu anayevurugisha dunia. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha