Mikoa na sehemu kadha wa kadha zaongeza mshahara kwa zaidi ya mia moja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2021

Tokea mwaka huu, mikoa na maeneo kadha wa kadha vimeongeza mshahara wa kila mwezi wa kiwango cha chini kabisa, ambao umeongezwa kwa zaidi ya Yuani mia moja, na kipato cha kila saa cha kiwango cha chini kabisa pia kimeongezwa .

Kuanzia tarehe mosi, Agosti mshahara wa kila mwezi wa kiwango cha chini kabisa hapa Beijing umeongezwa kuwa Yuani 2320 kutoka Yuani 2200, ambao umeongezwa kwa Yuani 120. Kipato cha kila saa cha kiwango cha chini kabisa kimeongezwa kuwa Yuani 13.33 kutoka Yuani 12.64.

Zaidi ya hayo, kuanzia robo ya pili mwaka huu, mikoa ya Jiangxi, Heilongjiang, Xinjiang Uygur, Shanxi, na Tibet kwa mbalimbali pia iliongeza mshahara wa kila mwezi wa kiwango cha chini kabisa kuwa Yuani 1850, Yuani 1860, Yuani 1900, Yuani 1950 na Yuani 1850.

Wakati huo huo, mikoa ya Anhui, Jilin, Sichuan, Guangdong, na Hainan ilipotoa habari husika za serikali za mwaka huu yote ilitaja mipango yao ya kurekebisha mshahara wa kiwango cha chini kabisa ndani ya mwaka 2021.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha