Kikosi cha 24 cha jeshi la kulinda amani la China katika DRC chatunukiwa “Nishani ya Amani”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2021

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Tarehe 12, Askari 218 wa kikosi cha 24 cha jeshi la kulinda amani la China katika DRC walitunukiwa "Nishani ya Amani" na Umoja wa Mataifa.

Kwenye hafla hiyo ya kutunukia nishani, amri jeshi wa Tume maalum ya Umoja wa Mataifa ya jeshi la kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (Kinshasa) Bw. Marcos De Sa Affonso Da Costa alisifu na kushukuru kazi za jeshi la kulinda amani la China kwenye eneo husika. Alisema kikosi cha askari wa uhandisi cha jeshi hilo kilichangia sana kazi ya jumla ya eneo la vita la kusini; na kikosi cha madaktari cha jeshi hilo kikikabiliwa na maambukizi mabaya ya Corona kilishikilia kutoa huduma za matibabu kwa askari wa majeshi ya kulinda amani, na wameonesha moyo wao wa kujitolea na mienendo mizuri ya kazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha