Kuadhimisha miaka 70 tangu Tibet kupata ukombozi wa amani, sanaa 86 za uchoraji wa picha na upigaji wa picha yaonesha mandhari ya Tibet inayopendeza sana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2021

Mchana wa Tarehe 21, Mei , ”Sura mpya ya maeneo ya theluji——Maonyesho ya uchoraji wa picha na upigaji wa picha ya kuadhimisha miaka 70 tangu mkoa wa Tibet kukombolewa kwa amani ”yalifunguliwa katika Jumba la makumbusho ya sanaa ya Yanhuang la Beijing. Kwenye maonyesho hayo, kulikuwa na sanaa 86 za sanamu、uchoraji wa picha kwa mafuta、uchoraji wa picha wa kichina na upigaji wa picha, ambazo zote zimeonesha sura ya Tibet katika karne mpya, zikionesha mandhari nzuri ya kupendeza ya Tibet, utamaduni wa Tibet na mtindo wa Tibet katika zama tulizonazo.

Ukumbi wa maonyesho. Picha ilipigwa na Lu Jing

Ukumbi wa maonyesho. Picha ilipigwa na Lu Jing

Watazamaji walioangalia sanamu ya“Zhuoma” iliyochongwa na msanii Sheng Yang. Picha ilipigwa na Lu Jing

Kwenye ukumbi wa maonyesho, sanamu ya“Zhuoma” iliyochongwa na msanii mzee Sheng Yang iliwavutia watazamaji. Sanamu hiyo ilionesha sura ya mlima wa theluji kwa kumaanisha moyo wa kabila la watibet , ikiwapa watazamaji taswira nyingi zenye maana pana. Na wasanii vijana pia walijitahidi kutengeneza sanaa zao kwa kusimulia vilivyo utamaduni wa watibet na mandhari nzuri ya Tibet katika zama mpya.

Mhusika alisema, maonyesho hayo yaliandaliwa pamoja na Shirika la Utamaduni wa China, Shirikisho la Wasanii wa uchoraji wa picha la China, Shirikisho wa Wapiga picha wa China na Shirika la Utamaduni wa Tibet, maonesho hayo yalifungwa tarehe 27, Mei.

 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha