Mkutano wa 44 wa Kamati ya Urithi wa Dunia wapitisha "Azimio la Fuzhou" likisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa

(CRI Online) Julai 19, 2021

Mkutano wa 44 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya UNESCO umepitisha "Azimio la Fuzhou" likisisitiza tena umuhimu mkubwa wa kuhifadhi urithi wa dunia na kuanzisha ushirikiano wa kimataifa na haja ya kufanya juhudi pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa .

Naibu waziri wa elimu wa China, ambaye pia ni mkurugenzi wa kamati ya kitaifa ya UNESCO nchini China na mwenyekiti wa Mkutano wa 44 wa Kamati ya Urithi wa Dunia, Bw. Tian Xuejun amesema, azimio hilo limeeleza kuwa urithi wa dunia ukiwa hazina ya kiutamaduni na kiasili, umetoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuhimiza mawasiliano ya utamaduni, amani ya dunia na maendeleo endelevu, huku likisisitiza tena jukumu la pamoja la binadamu la kukabiliana na changamoto mbalimbali za jadi na zisizo za jadi na kuhifadhi urithi wa dunia.

Azimio hili pia limetoa wito wa kufanya ushirikiano zaidi wa kimataifa chini ya utaratibu wa pande nyingi, kuzidisha uungaji mkono kwa nchi zinazoendelea hasa nchi za Afrika na nchi za visiwa vidogovidogo, na kuimarisha elimu kuhusu urithi wa dunia, utoaji wa ujuzi na matumizi ya teknolojia mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha