Vituo vya 5G zaidi ya laki 7.18 vimeanzishwa China na kuhusisha mikoa yote nchini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2021

Mkutano wa mawasiliano ya simu za mikononi wa kimataifa (MWC) umefunguliwa rasmi leo huko Shanghai. Naibu waziri wa viwanda na mawasiliano ya habari Bw.Liu Honglie alipotoa hotuba kwenye ufunguzi alisema, China imefanya juhudi za kusukuma mbele maendeleo ya teknolojia mpya na sekta ya mawasiliano ya simu za mikononi, na mafanikio ya kufurahisha yamepatikana. Uwezo wa mtandao wa internet umeendelea kuongezwa, uwekezaji umefikia zaidi ya Yuani bilioni 260; vituo vya 5G vipatavyo zaidi ya laki 7.18 vimeanzishwa nchini China, ambavyo vilichukua karibu asilimia 70 ya vile vya duniani; vifaa vya kimsingi vya 5G vimefikia zaidi ya milioni 20; sekta ya teknolojia imeendelezwa vizuri kwa haraka, na aina za simu za mikononi za 5G zimefikia 218, uuzaji wa simu za 5G ulichukua asilimia 90 kwenye soko la kiwango cha kati na cha juu.

Liu Honglie alisema, maendeleo na ufanisi wa simu za mikononi za 5G haviwezekani kutengana na juhudi za pamoja za sekta mbalimbali za jamii. Kati yao, kampuni za mawasiliano ya simu ya kimsingi zimefanya kazi kuu ya kujenga mtandao wa internet bila kujali athari ya maambukizi ya virusi vya corona, zimeharakisha ujenzi wa mtandao wa 5G, na kusukuma mbele maendeleo na matumizi ya sekta ya 5G.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha