Idadi ya wanawake kwenye bodi za wakurugenzi za taasisi kuu za mambo ya fedha za Uingereza yaongezeka na kuchukua theluthi moja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2021

Tarehe 19 Jumuiya ya washauri mabingwa ya Uingereza“Mambo Mapya ya Fedha”imetoa ripoti ikisema, katika miaka mitano iliyopita, idadi ya wanawake imeongezeka karibu imefikia theluthi moja kwenye bodi za wakurugenzi za taasisi zilizochukua nafasi 200 za mwanzo za Uingereza.

Ripoti ilisema, tangu mwaka 2016 wizara ya fedha ya Uingereza ilipoanzisha “katiba ya wanawake kushiriki kwenye mambo ya fedha”, idadi ya wanawake wa bodi za wakurugenzi za taasisi za fedha imeongezeka kutoka 23% hadi 32%, na kwenye kamati ya utendaji imeongezeka kutoka 14% hadi 22%.

Ripoti hii iliyothibitisha ushawishi wa“katiba ya wanawake kushiriki kwenye mambo ya fedha”kwa wanawake wanaoshughulikia mambo ya fedha ilikadiria kuwa, kufuata kasi ya ongezeko ya sasa, idadi ya wanawake kwenye bodi za wakurugenzi na kamati ya utendaji itachukua 50% mwaka 2029 na mwaka 2033.

“Japo idadi ya wanawake inaendelea kuongezeka kwa mwelekeo sahihi, lakini bado itafuata njia ndefu ,”mwandishi mmoja wa ripoti hiyo, ambaye ni mshirika wa “Mambo Mapya ya Fedha”Yasmin Chinwara alisema,“ sekta ya mambo ya fedha ikitaka kudumisha kasi hii ya mabadiliko ndani ya miaka mitano ijayo, inabidi ikabiliane na changamoto zaidi.”

Changamoto hizi ni kama vile, sekta ya mambo ya fedha inatakiwa kujenga njia ya kuingia kwa wanawake wenye vipaji, kuhakikisha wanabeba majukuma kwenye taasisi na kuwateua wanawake wengi zaidi wafanye kazi zinazoweza kuleta faida.

Mapema mwezi huu benki kuu ya Uingereza, Benki ya England na ofisi ya usimamizi wa vitendo katika mambo ya fedha zilisema, zinatumai kuharakisha anuai ya mji wa mambo ya fedha wa London,I anuai hiyo itasaidia kuongeza usalama na hatua madhubuti za benki za Uingereza na taasisi za uwekezaji .

Idara ya usimamizi wa mambo ya fedha inatumai anuai ya jinsia, makabila na kiwango cha elimu itaboresha mawazo ya aina mbalimbali ya kampuni za mambo ya fedha za kiwango cha juu.

Ofisa mtendaji mkuu wa Idara ya usimamizi wa vitendo katika mambo ya fedha Nikil Lati alisema:“Tuna wasiwasi kuwa, upungufu wa anuai na shirikishi ndani ya kampuni vitadhoofisha ubora wa maamuzi.”

Gazeti la“The Guardian”la Uingereza lilitoa habari zikisema, kampuni nyingi zaidi za mambo ya fedha za Uingereza zimeweka lengo la kuwa na anuai na shirikishi, kuchukua hatua ya kulinganisha mshahara wa msimamizi mwandamizi na hali ya utekelezaji ya timu ya shirikishi.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha