Mavuno ya majira ya joto ni Matunda Matamu!

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2021
Mavuno ya majira ya joto ni Matunda Matamu!
Tarehe 19, Julai, wakulima walichuma Matunda Matamu katika kijiji cha Xingsheng cha mji wa Shoucheng wa wilaya ya Minqin.(Picha ilipigwa kwa droni.)

Wakati wa mavuno ya majira ya joto, Matunda Matamu kwenye mashamba ya hekta zaidi ya elfu 13 katika wilaya ya Minqin ya mji wa Wuwei, mkoani Gansu yameiva mfululizo, ambapo kwenye mashamba, na soko la biashara pamejaa harufu nzuri ya Matunda Matamu. Tangu yalipofanya majaribio ya kupanda matunda hayo katika miaka ya 1960, mashamba ya upandaji wa Matunda Matamu ya Minqin yamepanuka siku hadi siku, na aina zake pia zimeongezeka na kufikia 108 za matawi matano, na utoaji wake unatazamiwa kuzidi tani laki 4 mwaka 2021. Hivi sasa, kutokana na upandaji wa matunda hayo kwenye mashamba makubwa pamoja na uuzaji wake wa njia mbalimbali, Matunda Matamu ya Minqin si kama tu yananunuliwa vizuri nchini, bali pia yanasafirishwa duniani, na imekuwa “sekta nzuri” inayoleta faida kubwa na kustawisha vijijini vya huko.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha