China yafaulu kurusha satelaiti D ya Tianhui No.1

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2021
China yafaulu kurusha satelaiti D ya Tianhui No.1

Saa 6:01 mchana wa Tarehe 29, Julai, China imefaulu kurusha satelaiti D ya Tianhui No.1 kwa maroketi ya D ya Changzheng No.2 kwenye obiti iliyopangiwa kwenye anga ya juu kutoka kituo cha kurusha satelaiti ya Jiuquan. Kazi hii ya kurusha satelaiti imepata mafanikio mazuri.

Habari zilisema, hii ni mara ya kwanza kwa maroketi ya D ya Changzheng No.2 kutumia mfumo mpya wa kudhibiti na kurusha satelaiti kwenye ardhi katika kituo cha Jiuquan, mfumo huu unaweza kukidhi mahitaji ya majaribio ya teknolojia ya kurusha maroketi ya D ya Changzheng No.2 na ya Changzheng No.4, na mfumo huo ni mdogo, wa kujiendesha, na usiosimamiwa na mtu, hii inarahisisha ufumbaji wa

mfumo wa kudhibiti na kurusha satlaiti kwenye ardhi, kuungana na mchakato unaoboreshwa siku hadi siku wa kudhibiti na kurusha, na kuongeza ufanisi wa kazi.

Roketi ya D ya Changzheng No.2 inayofanya kazi hii ni roketi ya ngazi ya pili ya majimaji yenye joto la kawaida, ambayo ilitengenezwa na Idara ya 8 ya kampuni ya kundi la teknolojia ya usafiri kwenye anga ya juu la China, uzito wake wa msukumo unafikia tani 300, uwezo wake wa kubeba ni tani 1.2 ikilinganishwa na obiti ya duara ya kilomita 700 ya jua, ina uwezo wa kurusha satelaiti moja au kadhaa hadi kwenye obiti tofauti. Hii ni mara ya 54 ya kurushwa kwa maroketi ya D ya Changzheng No.2 ya kubeba satelaiti, pia ni mara ya 381 ya kurushwa kwa maroketi ya Changzheng ya kubeba satelaiti.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha