Wastani wa ongezeko la mwaka la uwekezaji wa utafiti wa kimsingi wa China wafikia 16.9%

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 03, 2021

Tarehe 27, waziri wa sayansi na teknolojia, Bw.Wang Zhigang alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China kuwa, uwezo wa uvumbuzi wa asili wa teknolojia wa China umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Uwekezaji wa utafiti wa kimsingi umeongezeka kwa kasi, wastani wa ongezeko la mwaka umefikia 16.9%, kwa mara ya kwanza nafasi ya utafiti wa kimsingi imechukua zaidi ya 6% ya uwezekaji wa utafiti, kiwango cha utafiti wa kimsingi kimeinuliwa sana, sekta za kemia, vifaa, fizikia zimeingia kwenye safu ya mbele duniani, pia zimepata matokeo mengi ya uvmbuzi wa sayansi na teknolojia yanayowakilishwa na utafiti wa mawasiliano ya quantum na superconductor.

Baada ya kufanya juhudi kwa miaka mingi, kiwango cha utafiti wa kimsingi cha China kimeinuliwa sana kwa jumla, na ushawishi wake pia umeongezeka sana duniani. “China imekuwa nchi ya pili inayochangia zaidi makala za taaluma ya teknolojia za kiwango cha juu duniani. Katika sekta 12 zikiwemo vifaa, kemia, teknolojia ya mradi, hisabati, fizikia na kadhalika, makala za tasnifu za kiwango cha juu za China zilizonukuliwa zimeingia kwenye nafasi mbili za mwanzo .” Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango ya kimkakati ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Bw.Xu alisema.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha