Matokeo ya “Ripoti ya nusu mwaka” ya uchumi wa China yavutia watu macho

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 04, 2021

Tarehe 15, Julai, Idara ya Takwimu ya Kitaifa ilitoa takwimu za uchumi wa nusu ya kwanza ya mwaka huu. Uchumi wa China ulipata matokeo mazuri tena.

Kwenye mkutano kuhusu hali ya uendeleaji wa uchumi uliofanywa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, Liu Aihua, msemaji wa Idara ya Takwimu ya Kitaifa ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya Takwimu ya Uchumi wa Kitaifa alisema, uchumi wa nusu ya kwanza ya mwaka huu uliendelea kufufua, uliimarishwa kwa hatua madhubuti na kuendelea vizuri kwa utulivu. Wakati huo huo, ufufukaji wa uchumi wa nchini haujakuwa na uwiano, bado tunatakiwa kufanya jitihada ili kuimarisha msingi wa kufufua hali ya maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha