Watumiaji wa mfumo wa Harmony wa Huawei walioinuliwa ngazi wazidi milioni 50

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2021

Kampuni ya Huawei ilisema, hadi tarehe 6, Agosti, watumiaji wa mfumo wa Harmony wa Huawei walioinuliwa ngazi wamezidi milioni 50.

Mfumo wa Harmony wa Huawei ulitangazwa rasmi tarehe 2, Juni, mwaka huu. Wahusika walijulisha kuwa, mfumo huo ni wa kizazi kipya cha mfumo wa utendaji kwenye msingi wa akili bandia. Mfumo huu ni wepesi zaidi, kasi zaidi na usalama zaidi. Mfumo huu wa seti moja tu unaweza kukidhi mahitaji ya vifaa vingi kwa kupitia teknolojia ya kugawanywa.

Mwanzoni mwa Julai, mwaka huu, Huawei ilisema idadi ya watumiaji wa mfumo wa Harmony walioinuliwa ngazi ilifikia milioni 30, kwa wastani, katika wakati wa kila sekunde kuna watumiaji wanane wa mfumo huo walioinuliwa ngazi.

Huawei ilisema, hivi sasa simu za Huawei za aina zaidi ya 20 zinaweza kusasisha mfumo wa Harmony. Mdiea, iFlyetek, SUPOR na kampuni nyingine zaidi ya 300 zinashirikiana na mfumo wa Harmony. Inakadiriwa kampuni maalumu zaidi ya 40 zitakuwa milango mipya ya utumiaji wa mfumo wa Harmony.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha