Uwanja wa Kitaifa wa China “Kiota cha Ndege” utakuwa wa kufanyia sherehe ya kufunguliwa na kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya majira ya baridi ya Beijing 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2021

Michezo ya 32 ya Olimpiki ya majira ya joto imefungwa, wakati wa Michezo ya Olimpili umeingia ratiba ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing. Tarehe 9, Septemba, kampuni inayomilikiwa kitaifa ya Beijing, ambayo ni kampuni inayobeba jukumu la kujenga na kukarabati majengpo matatu ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya “Kiota cha Ndege”, “Mchemraba wa Maji” na “Ukanda wa Barafu”, inaeleza kwamba, wakati wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya majira ya baridi ya Beijing 2022, sherehe ya kufunguliwa na kufungwa kwa michezo zitafanyika kwenye Uwanja wa Kitaifa wa China (Kiota cha Ndege), hivi sasa Kiota cha Ndege kimeingia katika kipindi cha ujenzi na ukarabati, ambao utakamilika Oktoba, mwaka huu kwa mpango uliowekwa.

Tangu “Kiota cha Ndege” kilipofunguliwa kwa umma Septemba, 2008, kilionesha mvuto wa jengo hilo la Michezo ya Olimpiki na utamaduni wake kwa kupitia shughuli za utalii, tangu kufunguliwa kwake mpaka hivi leo, kimewapokea watalii zaidi ya milioni 35, na kimekuwa kivutio cha kutukuza utamaduni wa Michezo ya Olimpiki na Moyo wa Olimpiki.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha