Kuendeleza nishati ya bahari ili kusaidia kutimiza lengo la kupunguza utoaji wa kaboni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2021

Utekelezaji wa sera na hatua za kupunguza kodi na ada, kutia moyo kazi ya uvumbuzi, na kutoa uungaji mkono katika mambo ya fedha umesaidia ufufukaji wa uchumi wa bahari kwa pande zote.

China imekuwa soko kubwa la pili la uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo baharini katika dunia. Hivi sasa uwezo wa mashine za uzalishaji wa umeme kwa nishati ya mawimbi makali wakati maji hujaa na kupwa baharini umefikia kilowati 3820, ambazo zinachukua nafasi ya pili duniani. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, utoaji wa mafuta ghafi na gesi asilia baharini uliongezeka kwa asilimia 6.9 na asilimia 6.3 ukilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo shughuli zote za jadi za bahari zinaharakisha kubadilishwa muundo na kuwa za kutoleta uchafuzi mwingi kwa mazingira.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha