Fedha mtandao za Renminbi zitaonekana katika Kanivali ya Mambo ya Fedha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2021

(Jumba la kufanya Mkutano wa Biashara ya Huduma wa Kimataifa wa China wa mwaka 2021. Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Maonesho maalumu ya huduma za mambo ya fedha kwenye Mkutano wa Biashara ya Huduma wa Kimataifa wa China wa mwaka 2021 yatafanyika katika Bustani ya Shougang mjini Beijing kuanzia tarehe 3 hadi 7, Septemba. Maonesho hayo yatawavutia watu zaidi kwa hali yake mbalimbali. Licha ya kuweka maeneo manane makuu ya maonesho, shughuli mfululizo za Kanivali ya Mambo ya Fedha mtandao zitafanyika pia, ambapo Barabara ya Fedha mtandao za Renminbi itawekwa katika bustani hiyo, ambayo itawapa urahisi watazamaji kujaribu kununua vitu kwa kutumia pesa mtandao papo hapo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha