Mtazamo mpya huchochea ukuaji na ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2021

Rais Xi Jinping akitoa hotuba muhimu kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Boao la Asia (BFA) wa mwaka 2021. (Picha/Xinhua)

Maofisa na wataalamu wamesema, rais Xi Jinping ameiongoza China kuonyesha dhamira yake mpya na kuweka mwongozo wa sera mpya katika matukio kadhaa ya kidiplomasia mwaka huu, ili kusaidia kuchochea ufufukaji wa uchumi duniani, kuimarisha mshikamano na kudumisha umoja wa pande nyingi.

Juhudi hizi, ikiwemo kuleta mawazo mapya ya kukabiliana na maswala makubwa kama janga la COVID-19, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji usio na uwiano, zimetumika kama sehemu ya mabadiliko ya kudumu ya Mawazo ya Xi Jinping juu ya masuala ya Diplomasia, na kuonesha jukumu kubwa la China kama nchi kubwa inayoendelea.

Kitabu kinachohusu kujifunza Mawazo ya Rais Xi kilichapishwa Jumatatu ambacho kinaonesha falsafa mpya ya China kwenye sera ya mambo ya nje na diplomasia tangu Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika.

Wazo hilo ni nguzo ya msingi ya diplomasia kwenye zama mpya na ni mwongozo wa kivitendo.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Xi amejishughulisha na ratiba ngumu ya kidiplomasia ili kuendeleza ushirikiano na kuimarisha makubaliano kupitia shughuli mbalimbali za kidiplomasia, na kuchangia maoni na mipango mipya kwenye wazo hilo.

Hadi kufikia Jumatatu, Rais Xi alihudhuria mikutano muhimu 11 ya pande nyingi au pande mbili kwa njia ya video kwa mwaka huu.

Katika kipindi hichohicho, alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi 49 wakiwemo wakuu wa nchi, wakuu wa serikali au wakurugenzi wa mashirika ya kimataifa.

Ili kuendeleza diplomasia, pia ameshiriki kwenye shughuli zaidi ya 50 kwa kutoa hotuba kwa njia ya video, kutuma ujumbe na kuandika barua.

Hasa, amehutubia mikusanyiko mingi mikubwa ya uchumi na mikutano ya kilele ili kuunga mkono juhudi za dunia katika kuhimiza ufufukaji wa uchumi baada ya kutokea kwa janga la Corona.

Hafla hizo pamoja na mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia linalohusu Ajenda ya Davos lililofanyika mwezi Januari na Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia wa mwezi Aprili.

Pia ametoa wito wa kuboresha ushirikiano wa chanjo duniani, hasa usambazaji wa haki wa chanjo katika nchi zinazoendelea, ili kusaidia kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Sera mpya za mambo ya kidipomasia na ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa ziliwekwa wakati rais alipohudhuria kwenye mikutano hiyo.

Kuimarisha mafungamano ya uchumi wa kikanda, kutumia fursa zinazotokana na uvumbuzi wa teknolojia duniani na kuboresha ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni miongoni mwa mapendekezo muhimu yaliyotolewa na rais kwenye mikutano hiyo.

Ili kuendeleza zaidi pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kwenye matukio mbalimbali ametaja umuhimu wa kukuza zaidi pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na kufanya njia ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” iwe “njia ya kuondoa umaskini na njia ya ukuaji ili kuchangia ustawi wa pamoja wa binadamu wote".

Naibu mwenyekiti mtendaji wa taasisi ya mambo ya kimataifa ya China, Ruan Zongze amesema, busara na mawazo ya hivi karibuni ya Rais Xi ya “kushughulikia changamoto duniani kwa pamoja na namna ya kukuza maendeleo ya pamoja wakati wa janga hilo, zinaonesha juhudi kubwa za nchi katika kuheshimu jukumu na wajibu wake katika jukwaa la kimataifa".

Bw. Ruan ameongeza kuwa mapendekezo hayo ya sera mpya yanatokana na azma ya China ya kuwa na umoja, haki na usawa, ambayo yanatambuliwa na kuheshimiwa duniani, na yamejaa Mawazo ya Rais Xi Jinping kuhusu diplomasia.

Akizungumzia haja ya China kufuata zaidi wazo la Rais Xi Jinping kuhusu Diplomasia ambayo yanakua siku hadi siku, msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Wang Wenbin amesema "hatua na mazoezi lazima viongozwe na mawazo na nadharia".

Bw. Wang alisema kwenye mkutano na waandishai wa habari uliofanyika Juni 30, nchi ikiongozwa na wazo, huduma ya kidiplomasia ya nchi imejenga mtandao wa ushirikiano duniani na kutoa mchango wa China kwenye mageuzi na kuboresha mfumo wa utawala duniani.

"Mazingira mapya" yamechunguzwa chini ya mwongozo wa Mawazo, kwa ajili ya China kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kunufaishana na nchi mbalimbali duniani, alisema Yang Jiechi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC.

China imeanzisha ushirikiano na nchi 108 na mashirika manne ya kikanda, na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, lililotolewa na Rais Xi, limetafsiriwa kuwa hali halisi kuwa ni "faida kubwa ya umma duniani", Yang alisema katika makala iliyotolewa na Gazeti la Umma mwezi uliopita.

Ustawi wa dunia ukiwa akilini

Bw. Yang alibainisha kuwa kama sehemu ya wazo la Rais Xi, mtazamo wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja "una umuhimu mkubwa na unahitajika kwa vitendo" kutokana na changamoto kubwa za dunia kama vile janga la Corona na mabadiliko ya tabia nchi.

Kufuatia wito wake alioutoa mwaka jana wa kujenga jumuiya ya watu duniani wenye mazingira mazuri, Rais Xi alipendekeza wazo la kujenga kwa pamoja jumuiya ya kuishi kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili wakati akihutubia Mkutano wa kilele wa kuhusu Hali ya Hewa mnamo Aprili.

Katika mkutano huo, pia alibainisha matakwa ya nchi ya kufikia kiwango cha juu cha utoaji wa kaboni hadi kufikia 2030 na kutimiza usawazishaji wa kaboni kabla ya 2060.

Bw. Yanga amesema, matangazo haya ni “ushahidi wa wajibu mkubwa wa China ikiwa ni nchi kubwa”.

Katika kipindi cha mwaka huu, Rais Xi alirejea azma ya China ya ushirikiano wa pande nyingi kama kauli mbiu kuu la diplomasia ya nchi wakati alipohutubia kwenye hafla kadhaa kubwa, ikiwemo sherehe ya maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Kikomunisti cha China mnamo Julai 1.

"Tutaendelea kutetea ushirikiano badala ya mapambano, kufungua milango yetu badala ya kuifunga, na kuzingatia manufaa ya pande zote badala ya kunufaisha upande mmoja," alisema Rais Xi.

Hotuba na maoni ya Rais Xi yamekuwa yakihimiza ushirikiano wa pande nyingi, kuidhinisha mashauriano kati ya nchi kwa usawa, na kupinga zama za Vita baridi, alisema Waziri wa Mambo ya nje Wang Yi.

Maoni haya "yameleta mtazamo chanya katika dunia ambayo imegubikwa na ukosefu wa utulivu na kutokuwa na uhakika na kuweka msingi mpya wa nadharia na vitendo wa pande nyingi", alisema Bw. Wang katika makala iliyotolewa kwenye gazeti la Study Times mwezi uliopita. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha