Kwanini Xi Jinping anafuatilia sana Saihanba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2021

Tarehe 23, Agosti, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama Xi Jinping alifika kwenye Mlima Yueliang wa Msitu wa Saihanba mkoani Hebei, akikagua mazingira ya asili ya msitu huo, na kusikiliza ripoti kuhusu kazi husika. Kwanini Katibu Mkuu Xi anafuatilia zaidi msitu huu?

 

Agosti 23, Katibu mkuu Xi Jinping alifika kwenye Msitu wa Saihanba akikagua mazingira ya asili ya msitu huo, kusikiliza ripoti kuhusu kazi ya kushughulikia mfumo wa mlima, mto, ziwa, nyasi na mchanga na hali ya usimamizi na utunzaji wa msitu, na aliwatembelea walinzi wa msitu. Baadaye alifika kwenye msitu wa Kumbukumbu ya Shanghai, akikagua hali ya ukuaji wa miti, kufahamishwa kuhusu watu wa eneo hilo la msitu kutukuza Moyo wa Saihanba na kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora.

Picha hii iliyopigwa Juni 27, 2021 inaonesha mandhari ya asubuhi ya Msitu wa taifa wa Saihanba. (Mpiga picha Yang Shirao wa Shirika la Habari la China Xinhua)

Katibu Mkuu atetea “Moyo wa Saihanba”

Katibu mkuu Xi Jinping anakumbuka siku zote Msitu wa Saihanba. Mwaka 2017, Xi Jinping alitoa agizo muhimu mahususi juu ya hadithi za kusisimua kuhusu wafanyakazi wa Msitu wa Saihanba mkoani Hebei.

“Katika miaka 55 iliyopita, wafanyakazi wa Msitu wa Saihanba wakiitikia wito wa Chama, walifanya kazi zenye taabu kubwa kwenye mbuga iliyotelekezwa, ambapo‘mavumbi ya mchanga wa manjano yalifunika anga, na ndege walikosa miti ya kutua’, lakini walijikita na kujitolea, wakavumbua mwujiza wa kubadilisha mbuga hiyo kuwa msitu wa kuvutia, vitendo vyao vimefafanua wazo la ‘milima yenye ustawi wa miti na mito yenye maji safi ndiyo milima na mito ya dhahabu na fedha’, wajenzi hao wameonesha Moyo wa Saihanba wa kukumbuka jukumu, kuanzisha shughuli bila kujali taabu kubwa, na kujiendeleza bila kuleta uchafuzi kwa mazingira.”

Bw. Xi aliwasifu sana “wasaihanba” kwa juhudi walizofanya kizazi hadi kizazi na mchango mkubwa waliotoa katika muda mrefu uliopita, na kusifu sana Moyo wa Saihanba. 

Saihanba ilikuwa mbuga kubwa isiyo na upeo ambayo ilitelekezwa na binadamu.

Saihanba iko kaskazini mwa Mkoa wa Hebei, sehemu hiyo inasifiwa kuwa ni “chanzo cha mito, maskani ya mawingu, dunia ya maua, na bahari ya msitu”. Lakini ardhi hii ya msitu yenye nguvu ya uhai, ilikuwa mbuga iliyotelekezwa ambapo kila mara ilifunikwa na mchanga kutokana na dhoruba katika miongo kadhaa iliyopita.

Katika miaka ya 50 ya karne iliyopita, Mji wa Beijing ulikuwa unaathiriwa mara kwa mara na dhoruba ya mchanga. Wizara ya misitu ya wakati huo iliamua kujenga msitu mkubwa kwenye ardhi ya Saihanba kaskazini mwa Mkoa wa Hebei, ili kubadilisha sura ya maumbile ya sehemu hiyo.

Mwaka 1961, wafanyakazi walifanya ukaguzi kwa siku tatu kwenye sehemu hiyo, ambapo waligundua msonobari mmoja asilia (Larix) uliokua vizuri peke yake kwenye eneo la Hongsong’wa, ambao umeonyesha kuwa, miti mikubwa inaweza kukua vizuri kwenye sehemu ya Saihanba. Ndiyo maana sehemu hiyo ilichaguliwa kuwa mahali pa kupanda msitu.

  

Huu ni msonobari uliogunduliwa wakati wa kuchagua mahali pa kupandwa miti. (picha ya data)

Mwaka 1962, shamba la kupanda miti kwa mitambo la Saihanba lilianzishwa rasmi. Mwezi Septemba wa mwaka huo huo, wafanyakazi 369 walifika Saihanba kutoka sehemu mbalimbali nchini, miongoni mwao wakiwemo wanafunzi wengi waliohitimu kutoka vyuo vikuu au vyuo vya kazi za ufundi.

Baada ya kuanzia kazi, wajenzi hao walikumbwa na hali ngumu sana bila kutazamiwa.

Siku za baridi za Saihanba ni nyingi sana, wastani wa baridi kwa mwaka ni ya nyuzi 1.3 sentigredi chini ya sifuri, na wakati wa baridi kali ilifikia nyuzi 43.3 sentigredi chini ya sifuri; theluji inaonekana kila mahali kwa miezi saba kila mwaka, na wastani wa siku zisizo na ukungu ni siku 64 tu kwa mwaka, na kila mwaka kuna siku 76 zenye upepo mkubwa wenye nguvu zaidi ya 6. Kutokana na kukosa uzoefu wa kupanda miti kwenye eneo la baridi kali na la mwinuko wa juu kutoka usawa wa bahari, hivyo miche ya miti iliyokua vizuri kati ya ile iliyopandwa katika miaka miwili ya mwanzo haikufikia hata 8%.

Lakini “wasaihanba” hawakuacha juhudi zao kutokana na taabu. Ili kuinua zaidi ufanisi wa upandaji wa miti, waliboresha mitambo ya kupandikiza miche kutokana na hali tofauti ya ardhi, siku baada ya siku walipata ustadi na kurekebisha njia ya jadi ya kuotesha miche kwa kufunika, mwishowe walifanikiwa kuotesha miche ya kukua vizuri.

Miti midogo iliyopandwa kwa mitambo kwenye shamba la Saihaba. (picha ya data)

Wafanyakazi wa wakati huo walipoona miti midogo iliyostawi kwenye shamba lao, walifurahi sana hata walikumbatiana na kulia kwa sauti kubwa.

Tangu hapo kazi ya kupanda miti ilianza kufanyika kwenye eneo zima la Saihanba, awali kazi ya kupanda miti ilianza kufanyika kila ifikapo majira ya mchipuko, baadaye ilifanyika katika majira mawili ya mchipuko na mpukutiko, wafanyakazi walifanya juhudi kubwa za kupanda miti, siku hadi siku mlima uliotelekezwa pia ulipandwa miti na kuwa wa rangi ya kijani.

Kuchimba na kuandaa mashimo ili kupanda miti kwa mitambo kwenye eneo la Saihanba.(picha ya data)

Mti mmoja uliogunduliwa wabadilisha Saihanba kuwa“bahari ya miti”

Katika miongo kadhaa iliyopita, “wasaihanba” wa vizazi vitatu vya wazee, watu makamo na vijana walipanda miti mingi na kufaulu kujenga msitu mkubwa zaidi duniani kwenye shamba lenye hekta zaidi ya elfu 67, ambapo zaidi ya 80% ya eneo hili sasa limefunikwa kwa miti, hii imezuia kwa mafanikio ardhi ya mchanga ya Hunshandak isienee kuelekea upande wa kusini, kila mwaka linahifadhi chanzo cha maji kwa mita milioni 274 za ujazo kwa ajili ya Mkoa wa Hebei, na kama kujenga kuta imara dhidi ya dhoruba ya mchanga kwa ajili ya Beijing na Tianjin, kweli huu ni muujiza wa kubadilisha mbuga iliyotelekezwa kuwa bahari ya msitu.

Msitu wa Saihanba ni maonesho halisi ya wazo la “milima yenye ustawi wa miti na mito yenye maji safi, ndiyo milima na mito ya dhahabu na fedha.” Mazingira mazuri ya msitu huo yameleta maendeleo ya kasi ya shughuli za utalii vijijini, hali motomoto ya migahawa ya wakulima, na utengenezaji wa mazao ya kienyeji ya huko, mapato ya jumla ya jamii ya huko yamefikia Yuani za RMB zaidi ya milioni 600, na kuhimiza kwa nguvu vijiji vya pembezoni mwake vijiendeleze pia na kuondoa umaskini.

Kwenye Mkutano wa 3 kuhusu Mazingira wa Umoja wa Mataifa, wafanyakazi wa Msitu wa Saihanba walipewa tuzo ya juu zaidi ya kulinda mazingira iliyotolewa na Umoja wa Mataifa—“Walinzi wa Dunia”. Mwaka 2021, kwenye mkutano wa kufanya majumuisho kuhusu nchi nzima kupambana na umaskini, Shamba la Msitu wa Saihanba la Mkoa wa Hebei lilisifiwa kuwa ni “Mfano wa kuigwa wa mapambano dhidi ya umaskini”.

Msitu uliojengwa na wasaihanba kutoka “msonobari mmoja” hadi upandaji wa miti kwenye shamba la hekta elfu 67, kweli kila mti unaweza kuonesha mchakato wa maendeleo ya ustaarabu wa mazingira ya asili ya China. Mabadiliko makubwa yaliyotokea kwenye mbuga ya Saihanba ni kielelezo cha China cha kuboresha mazingira ya asili na maendeleo ya sifa bora.

 

Picha hii iliyopigwa Juni 27, 2021 imeonesha mandhari ya asubuhi katika Msitu wa kitaifa wa Saihanba. (mpiga picha Yang Shiyao wa Shirika la Habari la China Xinhua)

“Ubao huo wa Chesi” moyoni mwa Xi Jinping

Kujenga ustaarabu wa mazingira ya asili ni kazi ya muda wa maelfu ya miaka, ni mchango tunaotakiwa kutoa katika zama tulizonazo, na watu wa kizazi hadi kizazi watapata manufaa. Moyoni mwa Xi Jinping siku zote kuna “Ubao mkubwa wa chesi” unaohusu namna ya kufuata njia ndefu ya kujiendeleza na kulinda mazingira ya asili pia.

Katika agizo lake kuhusu hadithi za kusisimua za wajenzi wa Msitu wa Saihanba, Xi Jinping alisisitiza kuwa, watu wa Chama kizima na jamii nzima wanatakiwa kuwa na wazo la kujiendeleza bila kutoa uchafuzi kwa mazingira, kutukuza Moyo wa Saihanba, kudumisha ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili, kufanya juhudi kizazi hadi kizazi, kusonga mbele siku bila kusita, kutoa mchango siku zote, kujitahidi kupata hali mpya ya binadamu kuishi katika hali ya kupatana na mazingira ya asili, kujenga nchi yetu kubwa iwe na sura nzuri zaidi, ili kuwaacha watoto na wajukuu wetu mazingira mazuri ya anga buluu zaidi, milima inayofunikwa kwa miti mingi zaidi, na maji ya mito ni safi zaidi.

Kadiri China inavyoingia katika kipindi kipya cha maendeleo, ndivyo ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili unavyoendelea kusukumwa mbele zaidi, lengo lake ni wazi zaidi, kigezo ni cha juu zaidi na nguvu imekuwa kubwa zaidi.

Xi Jinping alidhihirisha kuwa, katika kipindi cha utekelezaji wa “Mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano”, ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili wa China umeingia katika kipindi muhimu cha mwelekeo wa kimkakati wa kuweka mkazo katika kupunguza utoaji wa carbo, kuongeza ufanisi wa kupunguza utoaji wa takataka na carbo, kuhimiza kazi zote za kiuchumi na kijamii ziendelezwe bila kutoa uchafuzi mwingi kwa mazingira, na kuyafanya matokeo mazuri halisi yaonekane katika kuboresha mazingira ya asili. Na ni lazima kutekeleza wazo jipya la maendeleo kwa ukamilifu, usahihi na kwa pande zote, kushikilia mkakati kithabiti na kupanga mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii kwa mtazamo wa juu wa kuwafanya binadamu waishi katika hali ya kupatana na mazingira ya asili.

Safari hii Katibu mkuu Xi alikwenda Saihanba kufanya ukaguzi, si kama tu ni kuwasifu na kuwatia moyo “wasaihanba” kwa juhudi zao za kupambana na taabu na kutoa mchango bila kusita katika miongo kadhaa iliyopita, zaidi ni kuagiza wazi tena kuhusu kusukuma mbele ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili siku hadi siku. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha