Wazo la Rais Xi ni muhimu kwenye utawala kwa mujibu wa sheria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2021

Kushikilia uongozi wa Chama, kunasisitiza ujamaa wenye umaalumu wa China

Yakitokana na utawala unaotegemea sheria na kuendelezwa na Chama cha Kikomunisti cha China, wataalamu wanasema mawazo ya Rais Xi Jinping kuhusu Utawala wa kisheria yanaonesha mafanikio ya hivi karibuni ya kutumia nadharia za U-marx zinazoendana na jamii ya Wachina, huku zikifanya kazi kama mwongozo wa kimsingi wa utawala unaotegemea sheria katika nchi.

Wanasema, katika zama mpya, kushikilia ujamaa wenye umaalumu wa China sio tu kunategemea utawala unaotokana na sheria, bali pia mahitaji ya kushikilia uongozi wa Chama ili kuboresha utawala wa kisheria.

Mwezi Novemba, mkutano wa kazi zinazohusiana na utawala wa jumla wa kisheria ulifanyika mjini Beijing, ambao uliashiria kuanzishwa kwa Wazo na hadhi yake kuwa itikadi inayoongoza utawala kwa mujibu wa sheria nchini China.

Katika mkutano huo, Rais Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi, alitoa hotuba akielezea mahitaji 11 ya kutimiza kazi inayohusiana na utawala kwa mujibu wa sheria nchini.

Kushikilia uongozi wa Chama kuliorodheshwa kama hitaji kuu. Mahitaji mengine ni pamoja na kufuata mtazamo unaozingatia watu, kufuata njia ya utawala wa kisheria ya ujamaa wenye umaalumu wa China, kuzingatia utawala ulio chini ya msingi wa Katiba ya Nchi na kuunda timu bora zaidi ya wataalamu wenye uadilifu na uwezo wa kusimamia mambo ya kisheria.

Li Lin, mtaalamu mwandamizi wa utafiti kutoka Chuo cha Sayansi ya Jamii cha China, anachukulia Wazo la rais Xi kuwa ni hatua muhimu katika kukuza sheria ya ujamaa wenye umaalumu wa China.

Akasisitiza kwamba uongozi wa Chama ndio sehemu muhimu zaidi ya maendeleo kama hayo.

"Hitaji kuu la kushikilia uongozi wa Chama kwenye utawala wa jumla kwa mujibu wa sheria, lipo kwenye msingi wa wazo la Rais Xi. Ni la msingi na lenye umuhimu mkubwa ambalo linabeba jukumu muhimu katika kuendeleza utawala wa kisheria," Li alisema.

Kwa mujibu wa Katiba ya China, uongozi wa CPC ni kitu muhimu zaidi katika juhudi za kufuata ujamaa wenye umaalumu wa China. Hii ina maana siri ya kutawala nchi na kulinda mamlaka ya Katiba ya Nchi ni kushikilia uongozi wa Chama.

Li alisema pia kuna tofauti kubwa katika kuzingatia uongozi wa Chama kati ya utawala wa kisheria wa China na ule wa nchi za kibepari za Magharibi.

"CPC inafanya juhudi kuongoza maboresho ya utawala wa jumla kwa mujibu wa sheria na kujenga nchi ya kijamaa iliyo chini ya msingi wa sheria ili kuwaletea furaha watu wa China na kuhusisha taifa," Li alisema.

"Kwa maneno mengine, Katiba ya Nchi inaonesha hitaji la kushikilia uongozi wa Chama na utawala wa kisheria wa kijamaa," alisema. "Pia ni tofauti kati ya utawala wa kisheria wa China na ule wa mataifa ya Magharibi."

Zaidi, Katiba ya Nchi pia inafafanua msimamo wa utawala wa CPC, ikionyesha uongozi wa Chama katika utangulizi wake.

"China inatawaliwa na CPC huku vyama vingine vya kisiasa vikishiriki. Sio kama nchi za Magharibi ambazo zinatenganisha madaraka kati ya watendaji, wabunge na mahakama, na vyama tofauti vinapeana zamu," Li alisema. "Hii ni tofauti kubwa kati ya utawala wa kisheria wa China na ule wa nchi za kibepari za Magharibi."

Katika miaka ya karibuni, utawala ulio chini ya msingi wa sheria umekuwa mada kuu kwenye mikutano mbalimbali ya CPC na mipango ya kazi – huo ni ushahidi kwamba Chama kimekuwa kikizingatia kuendeleza utawala kwa mujibu wa sheria, na kwamba utawala unaotegemea sheria hauwezi kutekelezwa bila uongozi wake.

Tangu Mkutano mkuu wa 18 la wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC imehimiza utawala wa jumla unaotegemea sheria, ambao ulijumuishwa katika Mkakati wa Nne wa maendeleo ya nchi.

Sehemu nyingine tatu za mkakati huo ni kukamilisha uanzishaji wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote, kuhimiza mageuzi kwa kina na kusimamia kwa makini chama kujiendesha.

Mkutano wa Nne wa Kamati Kuu ya 18 ya CPC wa mwaka 2014 ulipitisha uamuzi wa kuhimiza utawala wa sheria.

Baada ya Mkutano mkuu wa 19 wa Taifa wa CPC wa mwaka 2017, Kamati Kuu ya CPC iliunda Tume yake ya Utawala wa Jumla wa Sheria na kufanya maamuzi makubwa juu ya kuboresha njia hii kwa pande zote.

Yang Weidong, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Siasa na Sheria cha China, alisema kuendeleza utawala wa kisheria kwa pande zote si jambo rahisi, "kwa hivyo CPC inapaswa kuendelea kuboresha uwezo wake katika utawala kwa mujibu wa sheria".

Kwa mujibu wa Yang, licha ya kufanya utafiti zaidi juu ya sheria, kamati za Chama katika kila ngazi pia zinapaswa kuongeza uwezo wa kushughulikia maswala ya kisheria wakati zikichukua hatua za kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa mfano, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kamati za Chama na serikali katika miji na wilaya katika mkoa wa Gansu zimeamriwa kuweka ujenzi wa kisheria katika mpango wao wa kazi wa kila mwaka, ikimaanisha kuwa maofisa wanahitaji kuripoti wanachofanya ili kuendeleza utawala wa kisheria hadi kufikia mwishoni mwa mwaka.

Zaidi ya hapo, mwongozo uliotolewa na mkoa wa Hunan mwezi Julai kuhusu uendelezaji wa jamii chini ya msingi wa sheria, uliwahitaji maofisa wa Chama na idara za serikali kuongeza mafunzo ya sheria, kujifunza kutumia maarifa yao ya kisheria na kutekeleza mambo yanayohusiana na sheria katika ripoti zao za kazi za kila mwaka .

"Kama kamati husika za Chama hazitachukua hatua ya kuendeleza utawala wa kisheria au kuwa na mienendo mibaya wakati wakifanya kazi, wale wanaohusika na kamati za Chama watawajibishwa." Yang alisema.

"Zaidi ya hayo, kila mwanachama wa Chama na jumuiya ya Chama ni lazima atii Katiba ya Nchi na sheria badala ya kutumia vibaya madaraka au kupindisha sheria kwa sababu ya binafsi," alisema.

Kukabiliana na changamoto na hatari za ndani na nje ya nchi, wanachama, haswa wale walio kwenye nyadhifa za juu, wanapaswa kujizuia zaidi na kuchukua jukumu la uongozi katika kujifunza, kutumia maarifa yao na kutekeleza sheria ili kuboresha uwezo wao wa utawala unaotegemea sheria, alisema.

Utafiti zaidi unahitajika

Kwa maoni ya Lin Hongwu, ili kufikia lengo la utawala ulio chini ya msingi wa sheria, ni lazima kusoma kwa kina wazo la Xi Jinping juu ya Utawala kwa mujibu wa Sheria.

Bw. Lin ni naibu mkuu wa kituo cha utafiti kuhusu Mawazo akishirikiana na Jumuiya ya Wanasheria ya China. Kituo hicho kilianzishwa Beijing Juni 26.

Kwa mujibu wa Lin, moja ya kazi kuu za kituo hicho kwa mwaka huu ni kupanua utafiti wa sheria na kuchapisha makala ambazo zinaweza kusaidia jamii kuelewa wazo hilo kwa urahisi zaidi. Pia kinapanga kuandaa wataalam wa sheria kutafsiri wazo hilo na kutumia majukwaa anuwai kufahamisha matokeo yake ya utafiti.

Pia, kitaitisha mkutano wa kimataifa utakaojadili utawala wa sheria ili kutoa uungaji mkono mkubwa wa kisheria kwa maendeleo makubwa ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na kutumikia vyema juhudi zilizo chini ya msingi wa sheria kwenye mambo ya nje, ameongeza.

Kituo hiki kina wataalamu 100 wa sheria, kati yao 35 ni wafanyakazi wa kudumu.

"Tutawatumia vizuri wataalam ili kuboresha utafiti wetu juu ya nadharia za sheria, na tunatumai watatusaidia kuelimisha watu wenye vipaji zaidi katika kuendeleza utawala wa kisheria," alisema.

Kwa kuzingatia Mawazo, kituo hicho pia kitakusanya vitabu mfululizo katika miaka mitano ijayo, ameongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha