Rais Xi Jinping akagua maendeleo ya uchumi usiosababisha uchafuzi, na kuhimiza ujenzi wa mazingira ya asili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2021

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya chama, Agosti 23, 2021 alifanya ziara ya ukaguzi kwenye Shamba la Msitu wa Saihanba, akikagua ukuaji wa miti na kufahamishwa kuhusu kutukuza Moyo wa Saihanba na maendeleo ya hali ya juu ya Msitu wa Saihanba. Rais Xi alifanya ziara kwenye eneo la msitu lilipewa jina la Wang Shanghai, aliyekuwa ofisa wa shamba hilo. (Xinhua / Li Xueren)

SHIJIAZHUANG, Agosti 24 (Xinhua) – Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jumatatu alisisitiza umuhimu wa kuendeleza uchumi bila kusababisha uchafuzi wa mazingira na kuendeleza maendeleo ya ikolojia.

Rais Xi alisema hayo wakati alipofanya ziara kwenye msitu wa kumbukumbu katika Shamba la Msitu wa Saihanba lililoko kaskazini mwa Mkoa wa Hebei nchini China.

Msitu wa kumbukumbu wa Shanghai ulipewa jina la Wang Shanghai, ofisa wa msitu wa Saihanba aliyefariki, sehemu ambayo ni chimbuko la "Roho ya Saihanba," neno ambalo linahusishwa na vizazi vya wafanyakazi kwenye shamba walioweka lengo kuu akilini, wakifanya kazi kwa bidii na kufuata maendeleo yasiyosababisha uchafuzi.

Wafanyakazi wamejitolea kwa miongo kadhaa kufanya kazi ngumu na kuunda muujiza kwa kubadilisha eneo la jangwa kuwa msitu mkubwa.

Alipokuwa akizungumza na wajumbe wa wafanyakazi wa shamba hilo, Rais Xi alisema, juhudi zao zimeweka mfano mzuri na zina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya ikolojia katika nchi nzima.

Rais Xi pia aliwahimiza wafanyakazi wa Shamba la Msitu wa Saihanba kupata uelewa wa kina juu ya uhifadhi wa mazingira ya asili na kuendelea na bidii zao kwa mafanikio mapya.

Rais Xi Jinping wa China, anazungumza na wafanyakazi katika msitu uliopewa jina la Wang Shanghai, ofisa wa marehemu wa shamba la msitu wa Saihanba, wakati wa ziara ya ukaguzi wa msitu katika eneo la kaskazini mwa Mkoa wa Hebei wa China, Agosti 23, 2021. (Xinhua / Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China anaangalia ukuaji wa miti na anasikiliza maelezo kuhusu kutukuza “Moyo wa Saihanba” na maendeleo ya hali ya juu ya Msitu wa Saihanba uliopewa jina la Marehemu Wang Shanghai, aliyekuwa ofisa wa eneo la msitu huo, kaskazini mwa Mkoa wa Hebei wa China, Agosti 23, 2021. Rais Xi alifanya ziara ya ukaguzi kwenye msitu huo Jumatatu. (Xinhua / Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha