Lugha Nyingine
Rais Xi: Kuanza kwa mwanzo mzuri
Picha iliyopigwa Mei 22, 2020 ikionyesha bendera kwenye Uwanja wa Tian'anmen na sehemu ya juu ya Jumba la mikutano ya umma la Beijing. (Picha: Xinhua)
BEIJING, Agosti 15 (Xinhua) - Mwaka wa 2021, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimetimiza miaka 100, na taifa limeanza kutekeleza Mpango wa 14 wa maendeleo ya Miaka Mitano, kuanza vizuri kujenga kikamilifu nchi ya kisasa ya kijamaa.
Chini ya uongozi wa Kamati Kuu ya CPC na Rais Xi Jinping akiwa kiini chake, China imeshuhudia ukuaji endelevu na thabiti wa uchumi tangu mwanzo wa mwaka. Mafanikio mapya yamepatikana katika maendeleo ya hali ya juu, na watu wa China wanafurahia utulivu wa mazingira ya kijamii.
Mwanzo mzuri
Mapema mwezi Januari, Rais Xi Jinping, alihutubia semina elekezi iliyofanyika kwenye chuo cha kamati kuu ya CPC.
Alitoa wito kwa maofisa zaidi ya 190 wa ngazi ya mkoa na mawaziri waliohudhuria, wajitahidi kuanza vizuri kujenga kikamilifu nchi ya kisasa ya ujamaa.
Karibu wiki mbili baadaye, aliongoza kikao cha kikundi cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, Rais Xi alisisitiza haja ya kuhakikisha maendeleo mazuri ya kiuchumi na kijamii kwa mwaka huu, kwani "hatua ya kwanza" ya Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano ni muhimu.
Kwa mujibu wa Rais Xi, wakati wa kipindi cha 14 cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, China inapaswa kufanya kazi kutimiza ahadi katika maeneo anuwai, pamoja na kuhimiza maendeleo ya hali ya juu, kukidhi matarajio ya watu ya maisha ya hali ya juu, na kufanikisha kujitegemea kwa sayansi na teknolojia. Nchi pia imeanza kuharakisha kuhusisha maeneo ya vijijini.
Rais Xi ametaka kuwe na kasi endelevu kwenye kufikia maendeleo. Na maendeleo yanatakiwa kuwa kwenye pande zote, kutoka ukuaji wa uchumi hadi utunzaji wa mazingira, sheria, na ulinzi wa taifa.
Maendeleo ya kiwango cha juu
Akisisitiza jukumu muhimu la kuendeleza dhana mpya ya maendeleo na kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu, Rais Xi alihimiza juhudi zaidi zifanyike ili kufikia maendeleo yenye ubunifu, yaliyoratibiwa, yasiyosababisha uchafuzi wa mazingira, yaliyo wazi na shirikishi.
Moja kati ya majukumu muhimu kwenye Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano ni kuimarisha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Mwaka huu, Rais Xi amekagua kampuni kadhaa za teknolojia, na kusisitiza mara kwa mara umuhimu wa kujitegemea na kujiimarisha kwenye uvumbuzi wa kiteknolojia wa hali ya juu.
Uwekezaji mkubwa tayari unaingia kwenye kuhimiza uvumbuzi na ongezeko la uchumi. Katika nusu ya kwanza ya mwaka, uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 12.7, wakati uwekezaji katika sekta ya teknolojia ya juu uliongezeka kwa asilimia 23.5.
Kutosababisha uchafuzi wa mazingira ni sifa ya maendeleo ya kiwango cha juu. Katika ziara zake zote za ukaguzi nchini hadi sasa kwa mwaka huu, Rais Xi amekuwa akisisitiza umuhimu wa ulinzi wa mazingira katika kila ziara yake.
Maendeleo pia yamepatikana katika nyanja nyingine. Nchi imepanua kufungua mlango kwa hatua madhubuti, na mwongozo wa kusaidia mageuzi ya kiwango cha juu na kufunguliwa kwa Eneo Jipya la Pudong huko Shanghai, na orodha hasi ya biashara ya kuvuka mpakani katika huduma katika mkoa wa kusini wa kisiwa cha Hainan.
Kwa ajili ya maisha mazuri
Maendeleo ya kiwango cha juu yanapaswa kuunganishwa kikamilifu na kukidhi matarajio ya watu ya maisha bora, alisema Rais Xi.
Wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Qinghai, Rais Xi alitembelea nyumba ya mfugaji wa Tibet Sonam Tsering, ambapo alifahamishwa kuhusu mabadiliko katika maisha ya Sonam Tsering, na akauliza juu ya matarajio yake katika siku zijazo.
"Basi tufanye kazi pamoja kwa ajili maisha bora," Xi alisema.
Katika ziara zake nyingine vijijini, Rais Xi alizungumzia juu ya maswala mengine ikiwa ni pamoja na ustawi wa kawaida, viwanda vya vijijini na sayansi ya kilimo. Sera za kuimarisha usalama wa nafaka, kuendeleza sekta ya uzalishaji wa mbegu na kilimo cha kisasa zimeanza kutolewa.
Katika nusu ya kwanza ya mwaka, mapato ya kila mtu kwa wakazi wa vijijini nchini China yalifikia Yuan 9,248 ($ 1,427), yakiongezeka kwa asilimia 14.1 kwa mwaka. Kasi ya ukuaji wa mapato ya wakazi wa vijijini ilikuwa asilimia 3.4 zaidi kuliko ile ya wenzao wa mijini.
Ili kushughulikia matatizo yanayohusu umma, mabadiliko kadhaa ya kisera yamefanywa, ikiwa ni pamoja na kupunguza mzigo wa wanafunzi, kuboresha sera za uzazi wa mpango, na kuboresha mfumo wa huduma za afya.
Kwa ajili ya dunia nzuri
Mwaka 2021, binadamu bado wanaendelea kupambana na COVID-19 na virusi vinavyobadilika. Dunia nzima pia inakabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika inayosababishwa na hatua za upande mmoja, kutengwa na mapambano. Lakini China imechagua kutoa mchango wake kwa ajili ya dunia bora.
Tarehe 5, Agosti, katika ujumbe wa maandishi kwa mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu ushirikiano wa chanjo ya COVID-19, Rais Xi alitangaza kuwa China itatoa dozi bilioni 2 za chanjo ya COVID-19 kwa dunia na itatoa dola milioni 100 kwa mpango wa chanjo duniani COVAX kwa mwaka huu .
Dhamira ya China ilikaribishwa na jumuiya ya kimataifa. Shirika la Afya Duniani lilitoa taarifa, kushukuru mchango wa China na kubainisha kuwa juhudi za China " zitasaidia kuokoa maisha ya watu katika dunia nzima."
Tarehe 25 Januari, kwenye Mkutano wa baraza la uchumi wa dunia uliofanyika kwa njia ya video wa Ajenda ya Davos, Rais Xi alitoa wito kwa dunia ukisema "wacha mwanga wa uhusiano wa pande nyingi uangaze njia kwa wanadamu."
"Shida zinazoikabili dunia ni ngumu na zina utatanishi. Namna ya kuondokana na shida hizo ni kwa kushikilia msimamo wa pande nyingi na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja," alisema Rais Xi.
Ili kuendelea kuwasiliana kwa karibu na dunia nzima wakati wa janga hilo, Rais Xi mwaka huu amefanya mawasiliano kwa njia ya simu mara 50 na viongozi wa nchi nyingine na wakuu wa mashirika ya kimataifa. Tarehe 6 Julai, pia alikutana karibu na viongozi zaidi ya 500 wa vyama vya kisiasa na mashirika kutoka nchi zaidi ya 160 , kutaka kubeba jukumu la kutafuta ustawi wa watu na maendeleo ya wanadamu.
"Tunaamini kuwa wakati maslahi ya binadamu wote yapo hatarini, ni lazima China isonge mbele, ichukue hatua, na ifanye kazi kusaidia kuondoa hatari hiyo," Alisema Rais Xi kwenye mkutano wa ajenda ya Davos.
Kuelekea malengo ya pili ya Milenia
Mwaka 2021 ni wakati muhimu ambapo wakati wa malengo mawili ya karne ya China yanakutana – yaani kujenga jamii yenye ustawi wa wastani kwa pande zote wakati CPC inaposherehekea miaka mia moja tangu kuanzishwa kwake, na kujenga nchi kubwa ya kijamaa ya kisasa kwa pande zote wakati Jamhuri ya Watu ya China itaadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwake, ufikapo mwaka 2049.
"Katika karne iliyopita, CPC imepata mafanikio ya kihistoria kwa niaba ya watu. Leo, inawahamasisha na kuwaongoza watu wa China katika safari mpya kuelekea kufikia lengo la pili la karne" Alisema Rais Xi Julai 1 kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 100 ya CPC. Hata hivyo safari hiyo sio rahisi kabisa.
Mwaka 2021 pekee, China ilikabiliwa na changamoto kubwa kwa pande zote za ndani na za kimataifa. Mafuriko yaliukumba mkoa wa Henan na kusababisha madhara makubwa. Maeneo mengi yalikumbwa na COVID-19. China ilipambana na hali ngumu kwenye uhusiano kati yake na Marekani, na kujilinda dhidi ya hatua za uingiliaji wa nje kwenye maswala ya Xinjiang na Mambo ya Hong Kong.
Lakini chini ya uongozi wa Rais Xi na kwa moyo wa ushupavu, watu wa China walionyesha ujasiri na kushinda shida zote na kusonga mbele.
Mwezi Aprili, alipotembelea mbuga ya kumbukumbu ya medani ya vita vya Mto Xiangjiang wakati wa safari ya masafa marefu katika miaka ya 1930, Rais Xi alikumbuka moyo wa ushupavu wa Jeshi jekundu wa kutokubali kushindwa.
"Tunapaswa kuzingatia imani kama hiyo wakati tunajitahidi kufikia lengo la pili la karne, na kutimiza ndoto ya Wachina ya kuhusisha taifa," Alisema Rais Xi.
Aina nane maarufu zaidi za maua ya Yunnan hakika kuna moja inayokushangaza zaidi
Korongo wacheza kwenye uwangja wa juu hali ya viumbe yaendelea vizuri mkoani Tibet
Rasilimali ya utamaduni yasukuma mbele ujenzi wa kijiji cha kupendeza cha Luquan mjini Shijiazhuang
Mji wa Zhengzhou warudia katika hali ya kawaida ya uzalishaji na maisha
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma