Kuelekea China yenye ustawi na isiyo na uchafuzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2021

Ni wachache tu wanaweza kukataa kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni tishio moja kubwa linalowakabili binadamu katika karne ya 21. Ushahidi umekuwa ukijionesha kwa miongo kadhaa ikiwemo kuyeyuka kwa barafu katika ncha za dunia, mawimbi ya joto, ukame na kuongezeka kwa maji ya bahari, ambavyo vinatishia maisha na uchumi wa mabilioni ya watu.

Utabiri wa jumuiya ya kimataifa ya wanasayansi uko wazi kabisa -- mambo yatazidi kuwa mabaya kama mataifa yote hayatafanya juhudi za pamoja kubadili hali ya joto.

Yote haya hayajasahauliwa na Chama cha Kikomunisti cha China, ambacho kinapanga sera za hali ya hewa kwa lengo la kujenga China ya kisasa, yenye ustawi na isiyo na uchafuzi.

Haya ndiyo malengo yaliyotajwa na Rais Xi Jinping katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa mwaka wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka jana, wakati aliposema China inalenga kufikia kiwango cha juu cha utoaji kaboni kabla ya mwaka 2030 na kufikia usawazishaji wa kaboni ifikapo mwaka 2060.

Hakuna nchi ambayo imekuwa na ujasiri au mipango madhubuti katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kama China.

Utoaji wa kaboni wa China ni karibu robo ya jumla duniani, na serikali inajua gharama ya kutofanya chochote ikiwemo kuongezeka kwa uchafuzi wa maji na hewa, kiwango cha chini cha maisha na afya mbaya.

China iliyosawazisha utoaji wa kaboni itakuwa na mchango mkubwa kwa hali ya hewa duniani. Kwa mujibu wa makadirio, kama China ikifikia lengo la kusawazisha kaboni ifikapo mwaka 2060, itaweza kupunguza joto duniani kwa nyuzi 0.2 hadi 0.3 sentingredi.

Hii inaweza isiendane na malengo ya Makubaliano ya Paris ya kupunguza joto ya kuongezeka kwa nyuzi 1.5 sentigredi hadi kufikia katikati ya karne hii lakini, ikiwa kama mmoja wa watoaji wakubwa wa kaboni duniani, China itatoa mchango mkubwa na inapaswa kutoa msukumo kwa nchi nyingine kuiga mfano wake.

Changamoto inayoikabili dunia haiwezi kupuuzwa. Ripoti ya shirika la bima la Uswisi Re imeelezea changamoto hiyo kuwa ni "ya kutisha".

Ripoti ya "Uhakikisho wa Ufumbuzi wa Kuondoa Kaboni" iliyotolewa Julai 8 ilisema viwango vya utoaji wa kaboni duniani vinahitaji "kupunguzwa hadi nusu ifikapo 2030, na kufikia sifuri ifikapo mwaka 2050 na kuendelea kutotoa kabisa katika nusu ya pili ya karne".

"Hii itahitaji tani bilioni 10 hadi 20 za utoaji hasi wa kaboni kwa mwaka na baada ya 2050. Kuongeza uondoaji wa kaboni lazima kuanzia sasa, sambamba na juhudi kubwa za kupunguza utoaji, "ilisema ripoti hiyo.

Christoph Nabholz, ofisa mkuu wa utafiti katika Taasisi ya Uswisi Re, alisema katika taarifa: "Kama tunataka kufikia malengo yaliyowekwa kwenye Makubaliano ya Paris ya mwaka 2015, uondoaji wa kaboni utahitaji kubadilika na kuwa sekta yenye dola trilioni nyingi tu sawa na thamani ya sekta ya mafuta na gesi ya leo. Uwekezaji mkubwa katika sekta hii changa lazima uanze sasa. Kushindwa kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi kunaweza kusababisha upotezaji wa Pato la Dunia kwa asilimia 18.… Kutochukua hatua si chaguo. "

Kulipa gharama

Kutimiza usawazishaji wa kaboni halitakuwa jambo rahisi na litakuja na gharama zake, lakini ni gharama ambazo serikali ya China uko tayari kulipia ili kuwa na nchi isiyo na uchafuzi.

China imeshajiweka kama mtengenezaji anayeongoza wa teknolojia zisizo na uchafuzi, kutoka magari ya umeme na paneli za jua hadi mitambo ya upepo, na nchi imejipanga vizuri kukidhi mahitaji ya dunia ya teknolojia safi.

Kufikia kusawazisha utoaji wa kaboni kabla ya mwaka 2060 kunalingana na lengo la karne la CPC la kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa yenye ustawi, nguvu, ya kidemokrasia, iliyoendelea kitamaduni, yenye masikilizano na nzuri.

Hii ndio sababu ya mageuzi mengi kuendelezwa katika miaka ya hivi karibuni yakilenga kuzuia na kudhibiti hatari kubwa, kuondoa umasikini, kudhibiti uchafuzi wa mazingira, na kuimarisha mageuzi ya kimuundo ya usambazaji ili kuhimiza maendeleo endelevu na yenye afya ya kiuchumi na kijamii.

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, serikali ya China inafuata Makubaliano wa Paris, ambayo yanataja ahadi za kila taifa. China haijataka kukatiza biashara yoyote na mataifa yaliyoendelea na imejiwekea dhamira ya usawazishaji wa kaboni.

Profesa Gao Chao, mtaalam wa sayansi ya mazingira katika Kitivo cha Sayansi ya Kijiografia na jiografia ya bahari, cha Chuo Kikuu cha Nanjing mkoani Jiangsu, alisema itaichukua Marekani zaidi ya miaka 50 kusawazisha kaboni kutoka kwenye kilele chake cha utoaji kaboni.

Kwa China muda kati ya malengo mawili yaliyowekwa utakuwa miaka 30 tu, kwa hiyo China ina muda mfupi sana wa kufikia lengo.

"China inaweza kupata uzoefu na kujifunza kutoka kwa nchi zilizoendelea, kutumia teknolojia za kisasa na kuweka sera zinazofaa kwa nchi yetu," alisema.

"Muhimu zaidi, China ina faida zinazoonekana dhahiri katika kuhamasisha rasilimali zote za kijamii ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira na uzalishaji."

Gao alisema jambo muhimu katika kufanikisha malengo haya ya utoaji kaboni kabla ya mwaka 2030 na usawazishaji wa kaboni ifikapo mwaka 2060 ni kuhakikisha athari mbaya ni ndogo. Hii inamaanisha kuzuia kuleta "madhara yoyote muhimu au dhahiri kwenye ukuaji wetu wa uchumi katika mchakato huo".

"Tunaweza kupunguza utoaji kwa kupunguza matumizi ya nishati kwa kila sehemu ya Pato la Taifa na kuendeleza zaidi teknolojia za kaboni chache na zisizo na kaboni kama vile upepo, maji na nishati ya nyuklia," alisema. "Ni muhimu kwa nchi kuhimiza mtindo wa maisha wa kutoa kaboni chache kupitia hatua mbalimbali za kisheria, sera na uchumi."

Gao alisema kusawazisha kaboni kutapunguza athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na athari ya uchafuzi na kuepusha athari zozote za majanga yasiyotarajiwa kwa "jamii ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ".

Pia kunaweza kuleta "mabadiliko ya kimapinduzi katika kielelezo cha maendeleo ya uchumi wa nchi yetu, na kuwa njia inayofaa kutimiza ukuaji endelevu kwa maana halisi".

Gao alisema: "Kama China inaweza kutimiza lengo lake la kusawazisha kaboni, kwa kiwango kikubwa, itategemea na kufanikiwa au kushindwa kwa juhudi zote za binadamu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Pia itaamua,kwa kiwango kikubwa, sura ya China kama nchi inayowajibika inaweza kujengwa katika mawazo ya watu duniani. "

Ripoti ya Taasisi ya Maendeleo ya Nje ya Uingereza imekadiria uwekezaji unaohitajika kufikia usawazishaji wa kaboni ifikapo mwaka 2060, ni jumla ya dola trilioni 14.725 za Marekani kwa miaka 30 ijayo, ikiwa ni wastani wa dola trilioni 4.9 kwa muongo mmoja na dola bilioni 490 kwa mwaka.

Kwa mtazamo huu, kichocheo cha fedha cha kundi la G20 cha mwaka 2008 kilifikia dola trilioni 1.1 za Kimarekani, na mchango wa China ni dola bilioni 586 za Kimarekani.

Mshindi mkubwa

Ripoti ya ODI, "Maoni Matano ya Mtaalam juu ya Ahadi ya China ya Kusawazisha Kaboni ifikapo 2060", iliyotolewa Machi 9 ilisema China inapanga kuwa mshindi mkubwa katika utoaji wa kaboni ya chini.

Cao Yue, mtafiti mwandamizi na ODI, alisema China "inaweza kuwa imejizatiti kwenye mpango wake mkubwa zaidi wa viwanda" na ahadi yake ya kufikia usawazishaji wa kaboni ifikapo mwaka 2060.

"Sio siri kwamba China ilianza kujikita na sera ya hali ya hewa kama njia ya kushughulikia matatizo ya ndani, haswa, wasiwasi wa usalama wa nishati, ikiwa na lengo dhahiri la kupata fursa za kiuchumi duniani," alisema katika ripoti hiyo.

Cao alisema: "Wazo hili limechochea sekta ya nishati mbadala kuwa kwenye nafasi ya juu duniani katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Likiangaliwa kwa jicho lingine, tangazo la hivi karibuni ni dhihirisho lingine la sera ya viwanda ya China ya miaka mingi."

Kielelezo cha maendeleo bora cha hivi karibuni ni kubadilisha wazo l la kuamuru mustakabali wa uchumi duniani kuwa na kaboni chache, teknolojia ya juu, na teknolojia ya habari, alisema.

Cao alisema nchi nyingine zitahitaji kujitahidi zaidi kama hazitaki kushindwa kwenye mbio za kuwa na maisha yasiyo na uchafuzi na yenye ustawi.

Tangu Rais Xi alipotoa hotuba kwenye Mkutano wa Baraza Kuu wa UM mwaka jana, mwongozo wa China kwenye usawazishaji wa kaboni umepata mvuto wakati mamlaka na sekta zote nchini zikiongeza juhudi za kuendeleza uchumi usiosababisha uchafuzi.

Peng Kui kutoka Taasisi ya Mazingira Duniani ya Beijing, alisema ana imani kwamba China inaweza kufikia lengo lake la kusawazisha kaboni ifikapo mwaka 2060.

Kazi haitakuwa rahisi na kutakuwa na "changamoto kubwa na hali isiyokua na uhakika", alisema Peng, meneja wa uhifadhi wa mazingira na mpango wa maendeleo ya jamii wa GEI.

"Kwa mifumo yetu madhubuti ya kisiasa, na njia zake za maendeleo ya uchumi zenye umaalumu wa Kichina, lengo linaweza kufikiwa kupitia hatua za kisayansi zilizopangwa."

Kwa mujibu wa Peng, ili kutimiza lengo, upunguzaji wa utoaji wa kaboni daima unapaswa kuwa mwelekeo mkuu. Zaidi ni kuwa na mipango ya sahihi ya kimkakati ya kisayansi na ya muda mrefu.

"Tunahitaji kuwa na zana madhubuti za ufuatiliaji na tathmini ili kufikia lengo," alisema.

"Wakati huo huo, ni muhimu kufanya mabadiliko kuelekea uchumi wa mzunguko na uchumi wa kutoa kaboni chache na kujenga mfumo wa taifa wa ulinzi wa mazingira ya asili pamoja na vizuizi vya usalama wa ikolojia."

Peng pia alitoa wito wa kuboresha mfumo anuwai wa usimamizi wa mazingira ya asili na kuhamasisha ushiriki wa watu wote katika maendeleo ya kaboni chache na ulinzi wa mazingira.

Kufikia lengo hili, kutaleta matokeo makubwa kwenye ukuaji endelevu na mazingira ya ikolojia ya China na dunia.

"Itakuwa moja ya ishara kuu kwamba nchi imepata maendeleo endelevu, na pia itakuwa ni kama mafanikio makubwa ya ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili wa China," alisema Peng.

Ikiwa ni nchi yenye watu wengi na iatakayokuwa na uchumi mkubwa zaidi katika siku zijazo, kupitia kutimiza usawazishaji wa kaboni, China itaweza kutimiza wajibu wake wa kulinda mazingira ya dunia, huku ikihakikisha maendeleo endelevu, na kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha uhifadhi anuai ya viumbe duniani ambayo inawezesha kuishi kwa masikilizano kati ya watu na mazingira ya asili, Peng alisema.

Wakati ukuaji wa uchumi wa China ulitokana sana na makaa ya mawe, China ambayo sasa ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa duniani katika nishati safi, inaongeza kasi yake ya kuhamia kwenye nishati nyingine, mbadala zikiwemo upepo na jua.

Mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano wa China (2021-25) ambao ulipitishwa na Bunge la Umma la China, kwenye kipindi cha mikutano miwili mjini Beijing mapema mwaka huu, unaonekana kwa wachambuzi wengi kama hatua muhimu ya harakati ya uhifadhi wa mazingira nchini China.

Kuanzia Februari, China ilitekeleza sheria za mpito za usimamizi wa kazi ya utoaji wa kaboni ambayo zimetungwa ili kupunguza utoaji wa kaboni kwa watumiaji wakuu wa umeme.

Jumla ya makampuni ya umeme 2,225 yamejumuishwa katika mradi huo. Maeneo mengi zaidi, kama sekta za uzalishaji chuma na aluminium, zitajumuishwa katika mradi huo katika siku zijazo.

Kampeni ya nishati safi pia iliwezesha umma kukumbatia mtindo wa maisha rafiki kwa mazingira ya asili, kama ilivyooneshwa kwenye mauzo yanayoongezeka nchini China ya magari ya nishati mpya.

Ripoti iliyotolewa Mei 21 na jarida la The Atlantic, ilisema kwamba sekta ya magari ya umeme ya China "imekuwa mbele ya Marekani, na kusababisha hofu kwamba Marekani imeanguka vibaya nyuma ya mpinzani wake mkuu katika sekta muhimu ya siku za usoni".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha