Xi Jinping Aendesha Mkutano wa 21 wa kuendeleza kwa kina mageuzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2021

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunsiti cha China Xi Jinping, mchana wa Agosti 30 aliendesha Mkutano wa 21 wa Kamati Kuu ya kuendeleza kwa kina mageuzi kwa pande zote. Mkutano huo ulithibitisha na kupitia “Maoni kuhusu kuimarisha mapambano dhidi ya ukiritimba na kuhimiza kwa kina utekelezaji wa sera ya kufanya ushindani kwa haki”,“Maoni kuhusu kufanya mageuzi na kukamilisha mfumo na utaratibu wa kuimarisha usimamizi salama wa vifaa vya kimkakati na vya kukabiliana na dharura”, “Maoni kuhusu kuzuia na kushughulikia kwa kina hali ya utoaji wa uchafuzi kwa mazingira”, na “Maoni kuhusu kuifanya kazi ya mahesabu na usimamizi ioneshe umuhimu wake kwa ufanisi zaidi”.

Katibu mkuu Xi Jinping alipoendesha mkutano alisisitiza kuwa, kuimarisha utekelezaji wa hatua za kupambana na ukiritimba na kuhimiza kwa kina ushindani wa haki, haya ni matakwa ya undani ya kukamilisha mfumo wa uchumi wa soko huria ya kijamaa.

Mkutnao huo umedhihirisha kuwa, tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama ulipofanyika, tumetoa sera na hatua mfululizo muhimu kuhusu kupambana na ukiritimba na ushindani usio wa haki, kukamilisha taratibu zinazohusika, huku tukiongeza nguvu ya usimamizi husika, na kuchunguza kisheria vitendo vya ukiritimba vya makampuni zilizohusika na vitendo visivyo vya haki katika ushindani, sasa ufanisi wa hatua ya mwanzo umeonekana katika kuzuia upanuzi wa mitaji usiofuata utaratibu, na ushindani wa haki kwenye soko unaelekea vizuri hatua kwa hatua.

Mkutano huo umeeleza, ni lazima tuhimize kithabiti kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, kulinda haki ya umilikaji wa mali na hakimiliki ya ubunifu, kuvifanya viwanda na makampuni viongeze uelewa wa kufanya ushindani kwa haki, na kuelekeza jamii nzima ilinde mazingira ya soko lenye ushindani wa haki, kuziba pengo la usimamizi, kuongeza ufanisi wa usimamizi, na kuongeza nguvu ya utekelezaji wa sheria katika usimamizi.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha