Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa kilele wa biashara ya huduma duniani

(CRI Online) Septemba 03, 2021

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye mkutano wa kilele wa biashara ya huduma kwenye Maonyesho ya biashara ya huduma ya kimataifa ya China ya mwaka 2021.

Rais Xi Jinping amesema, China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali, kuendelea kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kunufaishana,kunufaika pamoja na fursa ya maendeleo ya biashara ya huduma, na kuhimiza ufufukaji na ongezeko la uchumi wa dunia.

Rais Xi ameongeza kuwa, China itaimarisha ujenzi wa kanuni katika sekta ya huduma, kuunga mkono Beijing na sehemu nyingine kutangulia kufanya majaribio na utekelezaji kuendana na kanuni za makubaliano ya biashara huria ya kiwango cha juu, na kujenga eneo la vielelezo la biashara ya kidijitali. Aidha, China itaendelea kuunga mkono maendeleo ya makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati, kupanua mageuzi ya “Bodi Tatu Mpya”, kuanzisha soko la hisa la Beijing, na kuanzisha jukwaa la kuhudumia makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha