Maonesho ya magari ya kimataifa ya Munich yafunguliwa
Kuzingatia mpango wa mwasiliano barabarani ya siku za baadaye

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2021

Tarehe 7, Septemba, watu wanatembelea kibanda cha Huawei kwenye maonesho ya magari ya kimataifa ya Munich, Ujerumani. Picha ilipigwa na mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la China Xinhua, Lu Yang

Maonesho ya magari na usafiri wa akili wa kimataifa wa Ujerumani umefunguliwa tarehe 7, huko Munich, kampuni mbalimbali maarufu za kimataifa zitaonesha magari yao mapya zaidi na kutoa mpango wa mawasiliano barabarani ya siku za baadaye .

Kwenye maonesho ya magari ya kimataifa ya Munich, Ujerumani, watu wanatazama skrini kusikiliza chansela wa Ujerumani, Bi. Merkel anayetoa risala kwenye ufunguaji wa maonesho. Mpiga picha Lu Yang

Habari zilisema kuwa, maonyesho hayo yamevutia kampuni zaidi ya 700 zilizotoka duniani kushiriki, pamoja na wafanyabiashara wenye viwanda vya magari, wafanyabiashara wa utoaji wa vipuri vya magari na utoaji wa Tehama, ambapo shughuli zaidi ya 100 za kuonesha magari mapya zitafanyika kwenye maonesho hayo, ambayo yataendelea hadi tarehe 12, na siku tatu za mwisho yatafunguliwa kwa umma.

Tarehe 7, Septemba, watu wanatembelea kibanda cha magari ya Renault kwenye maonesho ya magari ya kimataifa ya Munich, Ujerumani. Mpiga picha Lu Yang

Kwenye maonesho hayo, watu wanatembelea kibanda cha magari ya Weipai, ambayo ni chapa chini ya kampuni ya gari ya Changcheng ya China. Mpiga picha Lu Yang

Hili ni gari linalotumika umeme la i3s la BMW kwenye maonesho hayo. Mpiga picha Lu Yang

Hili ni gari linalotumika umeme la EQE 350 la Mercedes Benz kwenye maonesho hayo. Mpiga picha Lu Yang

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha