Makutano kati ya Ukuta Mkuu na Njia ya Hariri ya Kale!
Tamasha la Kwanza la Utamaduni na Michezo ya Sanaa ya Kimataifa Litafunguliwa Septemba 15

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 09, 2021

Mafungamano ya michezo ya sanaa, na maelewano kati ya raia. Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la kiraia la utamaduni na michezo ya sanaa la kimataifa la Ukuta Mkuu ulifanyika asubuhi ya Tarehe 7 Septemba kwenye Jumba la vyombo vipya vya habari la Gazeti la Umma, tamasha hilo linaandaliwa pamoja na Serikali ya umma ya Mkoa wa Hebei, na Wizara ya utamaduni na utalii ya China.

Picha hii inaonesha mkutano na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” la 2021

Habari zinasema kuwa, wageni 600 hivi watashiriki kwenye tamasha hilo, wakiwemo wajumbe wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine husika yaliyoko China, mabalozi wa ofisi za ubalozi wa nchi mbalimbali nchini China na maofisa wanaoshughulikia mambo ya utamaduni na michezo ya Sanaa, mashirika ya utamaduni ya kiraia ya nchi husika za “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, makundi ya michezo ya Sanaa, wasanii, warithi wa michezo ya Sanaa ya jadi, pmoja na wajumbe wa mashirika ya shughuli za utamaduni nchini China, na makundi ya China ya maonesho ya michezo ya Sanaa ya kiwango cha juu.

Tamasha hilo litaonesha ipasavyo utamaduni na michezo ya Sanaa ya kiraia ya aina mbalimbali ya nchi zinazojenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, tamasha hilo litakuwa jukwaa la kufanya maingiliano na ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya utamaduni, ambapo yatahimiza nchi husika za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kujenga pamoja hali ya mafungamano ya michezo ya Sanaa na kupata maelewano kati ya raia wa nchi mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha