Katibu mkuu wa UN atoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na msukosuko wa kiafya na kupunguza umaskini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 13, 2021

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Jana katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alitoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, ili kukabiliana na msukosuko wa kiafya kote duniani na kupunguza umaskini na hali isiyo ya usawa.

Ofisa mwandamizi huyo wa UN alisema hayo kwa njia ya video katika Siku ya Ushirikiano wa Kusini na Kusini ya UN, ambayo inasherehekewa duniani kote tarehe 12, Septemba kila mwaka.

"Maambukizi ya Corona ni changamoto yenye utatanishi zaidi inayoikabili dunia yetu moja kwa moja. Maambukizi hayo yanaharibu mafanikio yetu yaliyopatikana si rahisi katika jamii,uchumi na mazingira", alisema Bw. Guterres. "Katika kipindi hiki cha taabu kubwa namna hii, mshikamano unaotegemewa kwa ushirikiano wa Kusini na Kusini umeonesha tena umuhimu wake kwa nchi zinazoendelea."

Aliongeza kuwa, "kutokana na dunia inavyozidi kuitikia kupambana na Corona na kujitahidi kurudi katika hali ya kawaida, kukabiliana na tishio kwa hali ya kuishi katika mabadiliko ya hali ya hewa, ushirikiano wa Kusini na Kusini na ushirikiano wa pembetatu ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote wa hapo kabla."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha