Ajali kubwa ya mawasiliano barabarani nchini Algeria yasababisha vifo vya watu 12

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 13, 2021

Tarehe 12, ajali kubwa ya mawasiliano barabarani ilitokea katika mkoa wa Naama, kaskazini magharibi mwa Algeria, mpaka sasa imesababisha vifo vya watu 12.

Habari zilizolewa na shirika la kiserikali la Algeria zilisema kwamba, tarehe 12 basi moja lililobeba abiria liligongana na lori la trela nusu mkoani Naama, ajali hii imesababisha vifo vya watu 12, na wengine 7 walijeruhiwa.

Rais Tebboune wa Algeria amewapa pole jamaa za watu waliofariki, na kutoa agizo la kuwaokoa waliojeruhiwa kwa nguvu zote

ziwezekanazo. Idara ya mawasiliano ya Algeria ilisema , sababu ya ajali inachunguzwa.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Idara ya mawasiliano ya Algeria, miezi 7 za kwanza ya mwaka huu, ajali za mawasiliano barabarani takriban elfu 15 zilitokea nchini humo, na kusababisha vifo vya watu 1,974, wengine takriban elfu 2 walijeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha