Kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2021

Mwanzoni mwa utelekezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango, Deng Xiaoping alitoa lengo la “kujenga jamii yenye maisha bora nchini China” hadi mwishoni mwa karne ya 20. Kwenye msingi huu, Mkutano Mkuu wa 16 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulitoa lengo la kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote katika miaka 20 ya mwanzo wa karne hii. Baadaye Mikutano Mikuu ya 16 na 17 ya Chama ilitoa matakwa mapya ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, yaani kuleta manufaa kwa watu wa pande zote za nchi, na watu wote wa China. Watu wote wa mijini na vijijini wanatakiwa kupata maendeleo kwa pamoja, na kujenga jamii yenye maisha bora kunatakiwa kufuata hali halisi ya kila sehemu.

Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama Xi Jinping alifungamanisha kazi ya kuwasaidia watu maskini na majukumu ya Chama na serikali kuu, nia ya kimsingi ya Chama, malengo na matakwa ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na hali ya undani ya Ujamaa, akifafanua kwa kina umuhimu na udharura wa kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi wajiendeleze na kuondokana na umaskini nchini China. Mkutano wa 5 wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya Chama uliagiza kuhakikisha watu wote maskini vijijini wanaondokana na umaskini kwa kigezo kinachofuatwa sasa nchini China hadi ifikapo mwaka 2020. Na Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China pia iliweka mpango bayana kuhusu kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

Kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote ni lengo la kwanza kwenye malengo ya “Miaka 100 ya Chama”, na “Miaka 100 ya Taifa”, ni mnara muhimu kwenye mchakato wa ustawishaji mkubwa wa Taifa la China, na lengo hilo linaongoza katika mpango wa mikakati minne ya kutekelezwa kwa pande zote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha