Baraza la Usalama lazitia moyo nchi husika zirudishe mazungumzo kuhusu Boma la Nile ya Buluu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2021

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Jumatano wiki hii, Baraza la Usalama la UN linazitia moyo nchi za Misri, Ethiopia na Sudan zirudishe tena mazungumzo kati yao juu ya Boma la Ustawishaji la Ethiopia lililoko kwenye Mto Nile ya Buluu.

Katika taarifa ya Mwenyekiti ya Baraza la Usalama, baraza la usalama linazitia moyo pande tatu zenye maslahi husika zikubali mwaliko wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kurudisha tena mazungumzo kati yao, ili kufikia haraka ziwezavyo makubaliano yenye nguvu ya uzuizi ndani ya muda unaozifaa kuhusu kujenga na kuendesha boma.

Baraza la Usalama linazitaka nchi hizo tatu zisukume mbele mchakato wa mazungumzo hayo chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika AU kwa njia ya kiujenzi na kushirikiana.

Baraza la Usalama pia limewatia moyo wachunguzi wanaoalikwa kwenye mazungumzo hayo na wachunguzi wengine wowote wanaowezekana kualikwa na nchi hizo tatu kwa kauli moja waendelee kuunga mkono mazungumzo hayo, ili kuhimiza kutatua matatizo makubwa ya kiteknolojia na kisheria. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha