Idara ya usalama ya Nigeria yawakamata wafungwa 114 waliotoroka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2021

Tarehe 14, idara ya utawala wa magereza ya Nigeria imethibitisha kuwa, idara ya usalama ya Nigeria imewakamata wafungwa 114 waliotoroka kutoka gereza moja lililoko jimbo la Kogi, katikati ya Nigeria.

Katika miezi hii ya karibuni, matukio ya mashambulizi ya watu wenye silaha yalitokea kwa mfululizo nchini Nigeria, yakiwemo shambulizi dhidi ya ofisi ya polisi na gereza. Tarehe 5, Aprili, gereza moja lilishambuliwa na watu wenye silaha huko Owerri, mji mkuu wa jimbo la Imo, kusini mwa Nigeria, ambapo wafungwa zaidi ya 1,800 walitoroka.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha