Utawala wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2021

Tunapaswa kukamilisha mfumo na utaratibu wa kazi ya utungaji wa sheria, kuwawezesha wananchi wengi zaidi washiriki kwa utaratibu kwenye utungaji wa sheria, kusikiliza kwa makini maoni kutoka pande mbalimbali, kuzifanya sheria zioneshe kwa usahihi matakwa ya maendeleo ya uchumi na jamii, kusawazisha vizuri uhusiano wa kimaslahi, na kuufanya utungaji wa sheria uoneshe kazi yake ya uongozi na uhimizaji.

Tunapaswa kuimarisha utekelezaji wa Katiba ya Nchi na sheria, kulinda utekelezaji wa pamoja, heshima na maamuzi ya mfumo wa sheria wa kijamaa, kujenga mazingira ya utekelezaji wa sheria ambao watu hawapendi kuvunja sheria, hawaruhusiwi kuvunja sheria na hawathubutu kuvunja sheria; sheria zote zilizopo ni lazima zifuatwe, utekelezaji wa sheria ni lazima uwe wa makini, na vitendo vya uvunjaji wa sheria ni lazima viadhibiwe. Ofisi za mambo ya utawala ni nguzo za kutekeleza sheria na kanuni, zinapaswa kuongoza utekelezaji wa sheria kwa makini, kulinda maslahi ya umma, haki na maslahi ya wananchi na utaratibu wa jamii. Watekelezaji wa sheria wanapaswa kutii sheria.

Mamlaka za ngazi mbalimbali na maofisa viongozi wanapaswa kuongeza uwezo wa kutumia wazo na njia za utekelezaji wa sheria kuwafanya watu wawe na maoni ya pamoja juu ya mambo ya mageuzi, kufuata kanuni za vitendo vya kujiendeleza, kuondoa migongano, na kuhakikisha masikilizano katika jamii. Tunapaswa kuimarisha usimamizi kwenye shughuli za utekelezaji wa sheria, kuondoa kithabiti uingiliaji haramu kwenye kazi za utekelezaji wa sheria, kuzuia na kuondoa kithabiti hali ya kujilinda katika mikoa na idara husika, kuadhibu kithabiti ufisadi, mwenye madaraka anapaswa kuwajibika, mwendesha madaraka ni lazima asimamiwe, na vitendo vya kuvunja sheria ni lazima viadhibiwe.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha