Ndoto ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2021

Kujenga nchi ya mambo ya kisasa ya Ujamaa iliyo ya ustawi, demokrasia, ustaarabu na masikilizano, na kutimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China, hii ni ndoto kubwa kabisa waliyonayo wananchi wa China tokea Vita vya Kasumba, na ni maslahi ya juu kabisa na ya kimsingi ya Taifa la China. Hivi leo, juhudi zote zinazofanywa na sisi watu zaidi ya bilioni 1.3 ni kwa ajili ya kutimiza malengo hayo makubwa. China iliwahi kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, baadaye kutokana na mapinduzi ya viwanda yaliyofanyika kwa hali motomoto duniani, jamii ya binadamu iliingia katika kipindi cha kutokea kwa mabadiliko makubwa, China ikapoteza fursa ya kihistoria ya kwenda sambamba na dunia iliyopiga hatua, hali hii ikaipelekea China ipate hali ya kukumbwa na pigo. Hasa baada ya Vita vya Kasumba, Taifa la China likajitumbukiza katika hali nzito ya umaskini na udhaifu, hata ikafikia hali ya kuhuzunisha ya kuvamiwa na kulazimishwa kukatwa eneo la ardhi. Historia hii ya kuhuzunisha kamwe haitaruhusiwa kurudi tena! Kujenga nchi ya mambo ya kisasa ya Ujamaa iliyo na ustawi, demokrasia, ustaarabu na masikilizano ni malengo yetu, pia ni wajibu wetu, ni wajibu wetu kwa Taifa la China.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha