Putin atahudhuria kwenye Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2021

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov alisema jana kuwa, rais Vladimir Putin wa Russia amepokea mwaliko wa China, na atahudhuria kwenye Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing ambayo itafanyika Februari, 2022.

Vyombo vya habari vya Russia vilitoa habari zikisema, Lavrov alitangaza habari hiyo huko Dushanbe, mji mkuu wa Tajikistan. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha