Ushirikiano wa biashara kwenye mtandao wa intaneti kati ya China na Afrika wasaidia ufufukaji wa uchumi wa Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2021

Hivi karibuni, kipindi cha kutembeza bidhaa za Afrika za biashara kwenye mtandao wa intaneti wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika la mwaka 2021 kimeanza kufanya kazi rasmi. Shughuli za kutembeza bidhaa zitaendelea kwa miezi mitatu. Upande wa waandalizi unataka kuanzisha jukwaa jipya la ushirikiano wa kuvuka mipaka kwenye mtandao wa intaneti kati ya China na Afrika kwa kuchukua fursa hiyo, na kusukuma mbele ukuaji wa ushirikiano wa uchumi wa kidijiti na njia za biashara kati ya Afrika na China.

Soko la biashara kwenye mtandao wa intaneti ni ndogo katika Afrika, lakini ushirikiano kati ya China na Afrika una nguvu kubwa ya kukua. Ripoti mpya zaidi ya Kampuni ya huduma ya kifedha ya kimataifa VISA ilionesha kuwa, kuanzia mwaka 2019 hadi 2020, katika kanda ya kusini mwa Afrika ya Jangwa la Sahara, thamani ya biashara kwenye mtandao wa intaneti imeongezeka kwa asilimia 42 ikilinganishwa na mwaka jana. Hivi sasa, biashara ya kimataifa kwenye mtandao wa intaneti ni mtindo mkuu katika soko la biashara kwenye mtandao wa intaneti la kanda hiyo. Soko hilo limeshirikisha jukwaa la kampuni kwneye mtandao wa intaneti kama vile Kilimall, ambayo ilianzishwa na mjasiriamali wa China mwaka 2014 nchini Kenya.

Mwanauchumi wa Zambia, ambaye ni Mkurugenzi wa kitivo cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Zambia alisema, kipindi cha kutembeza bidhaa za Afrika za biashara kwenye mtandao wa intaneti wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika la mwaka 2021 ni shughuli yenye umuhimu mkubwa. Biashara kwenye mtandao wa intaneti inasaidia kupunguza gharama, kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha