Tamasha la Utamaduni na Michezo ya Sanaa ya Kiraia ya Kimataifa la Ukuta Mkuu “Ukanda Mmoja, Njia Moja” 2021 Lafunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2021

Usiku wa Septemba 5, Tamasha la utamaduni na michezo ya sanaa ya kiraia ya kimataifa la Ukuta Mkuu “Ukanda Mmoja, Njia Moja” 2021, ambalo linaandaliwa pamoja na Serikali ya Umma ya Mkoa wa Hebei na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China limefunguliwa kwenye kituo cha mawasiliano ya kimataifa ya sanaa ya Njia ya Hariri ya Langfang, Hebei na mjini Qinhuangdao pia.

Wakati wa kufanyika tamasha hilo, shughuli mbalimbali zitafanyika kwenye kituo cha mawasiliano ya sanaa ya Njia ya Hariri ya Langfang. Kundi la Maonesho ya Michezo ya Sanaa la Dongfang limeonesha mchezo wa sanaa wa “Utamaduni wa Dunia Unaong’ara” kwenye ufunguzi wa tamasha hilo, wasanii wa kiwango cha juu walionesha vilivyo mvuto wa utamaduni wa mashariki ya dunia na mvuto wa anuwai wa utamaduni wa dunia.

Kwenye tamasha hilo, watu watatumbuizwa pia kwa michezo ya sanaa ya Opera maarufu duniani, michezo ya sanaa ya Opera ya Beijing, na maonesho kadha wa kadha yatakayowavutia kweli. Waandalizi wa tamasha hilo wameandaa pia maonesho ya michezo ya sanaa kwa njia ya video, ambayo yataanza kwa wakati mmoja kwenye tovuti ya kiserikali ya tamasha na tovuti ya gazeti la umma, maonesho hayo ya michezo ya sanaa ipatayo zaidi ya 20 ikiwemo “Agano ya Michezo ya Sanaa”, “Ngoma Kwenye Njia ya Hariri”, “Muziki Unaosikika Kwenye Njia ya Hariri”, na kadhalika hakika itawatumbuiza watazamaji kwa furaha.

Ufunguzi wa shangwe wa Tamasha la utamaduni na michezo ya Sanaa ya kiraia ya kimataifa la Ukuta Mkuu la Ukanda Mmoja utawaletea watazamaji wa nchini na wa ng’ambo uhondo wa utamaduni, ambao utaonesha hali ya mafungamano ya mataifa na makabila, na usanifu wa majengo na sanaa vinavyoendana.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha