Xi Jinping ashiriki kwenye majadiliano ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa na kutoa hobuba muhimu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2021
Xi Jinping ashiriki kwenye majadiliano ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa na kutoa hobuba muhimu

Rais Xi Jinping alishiriki kwa njia ya video kwenye majadiliano ya kawaida ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa jana tarehe 21, Septemba hapa Beijing, ambapo alitoa hotuba muhimu ya “Kuwa na nia thabiti, kushirikiana katika kukabiliana na changamoto, na kujenga pamoja dunia nzuri zaidi."

Rais Xi amedhihirisha, mwaka huu ni wa 100 wa Chama cha Kikomunisti cha China, pia ni mwaka wa 50 tangu Jamhuri ya Watu wa China iliporudisha kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa, China itaadhimisha kwa shangwe tukio hili la kihistoria. Tutaendelea na juhudi za kuhimiza ushirikiano kati ya China na Umoja wa Mataifa uelekee kwenye ngazi mpya, na kutoa mchango mpya mkubwa zaidi kwa ajili ya mambo makubwa ya Umoja wa Mataifa.

Rais Xi alisisitiza kuwa, katika mwaka mmoja uliopita, viongozi wa nchi mbalimbali walihudhuria mikutano mfululizo ya Maadhimisho ya Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, ambapo waliahidi kufanya ushirikiano katika kupambana na janga la Corona, kupeana mikono kukabiliana na changamoto, kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kuimarisha umuhimu wa Umoja wa Mataifa, na kujenga siku za baadaye za pamoja za watu wa vizazi vya sasa na wa vizazi vijavyo. Katika mwaka mmoja uliopita, mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika miaka mia moja iliyopita yalitokea duniani yakiambatana na maambukizi makubwa ya virusi vya Covid-19 na kuleta athari kubwa. Watu wa nchi mbalimbali wamekuwa na matarajio makubwa zaidi juu ya maendeleo ya amani, wakitoa sauti kubwa zaidi juu ya usawa na haki, na wamekuwa na nia thabiti zaidi ya kutafuta ushirikiano wa kunufaishana.

Rais Xi amesisitiza kuwa, hivi sasa maambukizi ya Corona bado yanaenea vibaya kote duniani, mabadiliko makubwa ya kina yametokea katika jamii za binadamu. Dunia imeingia kwenye kipindi kipya cha msukosuko na mageuzi. Kila mwanasiasa anayewajibika anapaswa kuwa na nia thabiti na ujasiri kwa kujibu maswali ya masomo ya zama tulizonazo, na kutoa chaguo la kihistoria.

Alisema, kwanza lazima tungejitahidi kupambana na maambukizi ya Corona, na kujipatia ushindi katika mapambano hayo makubwa yanayohusiana na mustakabali wa binadamu. Pili tunapaswa kuufanya uchumi urudi katika hali ya kawaida, kuhimiza uchumi wa dunia nzima uendelezwe vizuri kwa nguvu kubwa zaidi bila kutoa uchafuzi kwa mazingira, na kujitahidi kwa pamoja kuhimiza maendeleo ya dunia nzima ielekee kipindi kipya cha kuwa na uwiano, uratibu na shirikishi.    

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha