Rais wa Zanzibar Tanzania atunuku nishani kwa kikosi cha matibabu cha China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2021

Tarehe 21, Rais Mwinyi wa Zanzibar, Tanzania alitunuku nishani kwa wajumbe wa kikosi cha 30 cha matibabu cha China katika Ikulu ya Zanzibar kwa kusifu kazi yao nzuri ya matibabu huko.

Mwinyi aliisifu sana na kushukuru misaada mingi bila ubinafsi kutoka China tokea mwaka 1964, hususan katika sekta ya matibabu na afya. China ilikuwa imepeleka kikosi cha matibabu, kusaidia kujenga hospitali, kutoa vifaa vingi na dawa za matibabu, kutoa mafunzo ya matibabu kwa madaktari wa huko, kusaidia kukinga na kutibu malaria na magongjwa mengine ambayo inafanya kazi muhimu kabisa kwa maendeleo ya mambo ya matibabu na afya ya Zanzibar.

Konseli mkuu wa China huko Zanzibar Bw. Zhang Zhisheng alisema, China itaendelea kutoa msaada kwa Zanzibar kwa kadiri iwezavyo katika sekta ya matibabu na nyingine. Inapenda kuendelea kufanya juhudi pamoja na Zanzibar katika kuhimiza kujenga jumuiya ya uhusiano wa karibu zaidi ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.   

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha