Utafiti waonesha COVID-19 huenda kuambukiza nchini Marekani kuanzia Septemba, 2019

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 24, 2021

Watafiti wa China wamegundua kwa kupitia uchambuzi wa data kubwa kuwa, maambukizi ya Covid-19 huenda yalienea nchini Marekani kuanzia Septemba, 2019, ambapo ni mapema zaidi kuliko siku iliyotangazwa na serikali ya Marekani ya kuthibtishwa kwa mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya Covid-19.

Kwa mujibu wa makala iliyotolewa Jumatano wiki hii kwenye jukwaa la ChinaXiv, utafiti uliofanywa kwa mfululizo umeonesha kuwa, kabla ya kulipuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini China, dalili za kushambuliwa na virusi vya Corona zilikuwa zimeonekana katika nchi za Marekani, Hispania, Ufaransa, Italia, na Brazil.

ChinaXiv ni jukwaa la huduma ya uchapisho la intaneti linaloendeshwa na maktaba ya sayansi ya kitaifa ya Taarifa ya Sayansi ya China.

Makala hiyo yenye kichwa cha "Kufanya uchambuzi kwa Mtazamo wa Uwezekano kuhusu siku ya kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona" ilidhihirisha kuwa, uchambuzi uliofanywa kwa mujibu wa data zinazohusu hali ya siku zilizopita na ya siku zinazoendelea, na uchambuzi uliofanywa kwa mujibu wa mfano wa hisabati ili kupata viwango na tarakimu husika mbalimbali, unaweza kuonesha kanuni za maambukizi ya ugonjwa.

Watafiti walijenga mfano mmoja wa uboreshaji kwa kutumia mfano wa maambukizi ya ugonjwa na kutumia mbinu ya uchambuzi wa data kubwa, na kutokana na takwimu zilizotangazwa hadharani, walichambua siku ya mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya Covid-19 katika majimbo 12 ya sehemu ya kaskazini mashariki ya Marekani, mjini Wuhan na mkoani Zhejiang, China.

Matokeo ya utafiti yalionesha, siku ya kuambukizwa Corona kwa mgonjwa wa kwanza (uwezekano umefikia asilimia 50) ni kati ya Agosti na Oktoba, 2019 katika majimbo 12 ya Marekani, siku hiyo haiwezekani kuwa kabla ya tarehe 26, Aprili, 2019, ambayo ni ya mgonjwa wa Kisiwa cha Rhode, na pia haiwezekani kuwa baada ya tarehe 30, Novemba, 2019 katika jimbo la Delaware.

Tarehe zote zilizooneshwa kutokana na data ni kabla ya tarehe 20, Januari, 2020, ambayo ni siku iliyothibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa na virusi vya Corona, ambayo ni siku iliyotangazwa na serikali ya Marekani. Hii inathibitisha kuwa inaaminika maambukizi ya Corona nchini Marekani ilianzia Septemba, 2019.

Matokeo pia yameonesha, mgonjwa wa kwanza wa Corona mjini Wuhan, China kwa uwezekano uliofikia asilimia 50 alithibitishwa tarehe 20, Desemba, 2019, na mgonjwa wa kwanza aliyethibtishwa mkoani Zhejiang ni tarehe 23, Desemba, 2019. Kutokana na hali hii kuna uwezekano mkubwa kuwa maambukizi ya Corona yalianzia nchini China mwishoni mwa Desemba, 2019.

Makala hiyo ilisema, data hizo zinaendana na matokeo ya utafiti wa elimu ya magonjwa ya kuambukiza, hii inaonesha kuwa njia hii ya mahesabu ni sahihi inayoaminika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha