Algeria yatangaza kufunga usafiri wa anga kwa ndege za Moroko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 24, 2021

Tarehe 22, ikulu ya rais ya Algeria ilitoa taarifa ikisema kwamba, kutokana na “sera ya uhasama” dhidi ya Algeria iliyotekelezwa na Moroko, Algeria iliamua kufunga usafiri wa anga kwa ndege zote za Moroko kuanzia siku hiyo.

Tarehe 24, Agosti, waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Lamamra alisema, kutokana na “sera ya uhasama” dhidi ya Algeria iliyotekelezwa na Moroko kwa muda mrefu, Algeria imeamua kukatisha uhusiano wa kibalozi na Moroko kuanzia siku hiyo. Bw. Lamamra alisema, maofisa wa Moroko walioko kwenye Umoja wa Mataifa walichochea mgongano kwenye uhusiano kati ya makabila madogo ya Algeria na serikali ya Algeria, na kupeleka uhasama wa nchi hizi mbili ufikie kileleni.

Katika muda mrefu uliopita, kutokana na tatizo la Sahara Magharibi, uhusiano kati ya Algeria na Moroko umekuwa na hali ya wasiwasi, siku zote mpaka kati ya nchi hizi mbili unafungwa.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha