Viongozi wengi walaumu kukosekana kwa usawa katika ugawaji wa chanjo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2021

Tarehe 23, kwenye hotuba walizotoa kwenye mjadala wa kawaida wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa, viongozi wengi wa Afrika walilaumu hali isiyo ya usawa katika ugawaji wa chanjo za Corona, na walitoa wito wa kubadilisha haraka hali ya kushindwa kwa Waafrika wengi kupata chanjo zinazoweza kuokoa maisha yao.

Rais Geingob wa Namibia alisema, hali halisi ya kukosekana kwa usawa katika ugawaji wa chanjo ni mbaya sana, hata ikiwa kama “ubaguzi wa rangi wa chanjo”. Wakati wananchi wa baadhi ya nchi wanapewa dozi ya kuongeza nguvu, watu wa nchi nyingine bado wanasubiri dozi ya kwanza ya chanjo.

Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini alisema, zaidi ya asilimia 82 ya chanjo duniani zimenunuliwa na nchi tajiri, na chini ya asilimia 1 tu zimezipa nchi maskini. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushikilia kanuni ya ushikamano na ushirikiano kwenye suala la kuhakikisha watu wanapata chanjo za Corona kwa usawa.

Rais Samia wa Tanzania kwenye hotuba yake alisema, hali isiyo ya usawa katika ugawaji wa chanjo “inatushangaza”, huku akihimiza nchi zenye chanjo za ziada kutoa chanjo zao ili nchi nyingine zinufaike pamoja. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha