China yatoa waraka kuhusu “Safari ya China kutoka umaskini hadi ustawi”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2021

Ofisi ya Habari ya Baraza la serikali la China Jumanne hii hapa Beijing imetoa waraka kuelezea safari ya nchi hiyo hadi kufikia ustawi katika maeneo yote.

Waraka huo wenye kichwa “Safari ya China kutoka umaskini hadi Ustawi” linasema kufikia ustawi katika nyanja zote kama ilivyotangazwa mwezi Julai mwaka huu wa 2021, ni mwanzo muhimu kuelekea ustawishaji wa taifa la China.

Waraka huo unasema, “Kupatikana kwa ustawi kunatekeleza ndoto iliyopiganiwa kwa muda mrefu na Taifa la China.”

Wakara huo unapongeza juhudi za Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Wachina kwa ujumla na inaonyesha China kufanikiwa katika kufikia ustawi kupitia maendeleo ya pande zote kwa wote.

“Kufikia ustawi kumehitaji uvumilivu wa hali ya juu na inadhihirisha mafanikio makubwa kwa CPC na Wachina kwa ujumla” inasema.

Kuhusu kufikia ustawi katika nyanja zote kama mchango mkubwa wa China kwa Dunia, waraka huo pia umeeleza namna Dunia itanufaika kutokana na ustawi wa China.

“Ikiwa nchi yenye idadi kubwa ya watu na nchi kubwa inayoendelea, China imechangia kwenye amani ya dunia na maendeleo kwa kufikia ustawi katika mambo yote”.

Katika kufikia jamii yenye maisha bora, China imesaidia kwa kasi kikubwa kupunguza idadi ya watu maskini duniani na kupata uzoefu mpya katika kujenga mambo ya kisasa kwa binadamu, huku sera yake ya ufunguaji wa uchumi wake imeleta ushirikiano wa kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha