Fainali za Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya maandishi ya kichina ya Hanzi” kwa mwaka 2021 kuanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2021

Fainali za Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya maandishi ya kichina ya Hanzi” kwa mwaka wa 2021 ambazo zinaandaliwa na “Shirikisho la watu wa China kwa Urafiki wa nchi za kigeni” na kuendeshwa na Tovuti ya Gazeti la Umma na Serikali ya mji wa Xining yamepangwa kufanyika tarehe 12 ya Mwezi Oktoba mwaka huu wa 2021 huko Xining, mji mkuu wa mkoa wa Qinghai nchini China.

Baada ya duru kadhaa za ushindani mkali, ambapo video ziliwasilishwa katika onesho lililofanyika kwa njia ya mtandao, washindi 10 ambao video zao zilichaguliwa kuingia kwenye hatua ya nusu fainali walichaguliwa na kamati ya maandalizi kuendelea kwenye hatua ya fainali. Washiriki walioingia kwenye hatua hii ya fainali wanatoka katika nchi za India, Syria, Zimbabwe, Japani, Jamhuri ya Kongo, Kazakhstan, Marekani, Argentina, Ufaransa na Ujerumani.

Kila mshiriki wa fainali atatoa hotuba ya dakika 7 kwa kulenga kaulimbiu ya neno la kichina ‘Ren’ ambalo linawakilisha ukarimu na umoja wa vitu vyote chini ya mbingu, thamani ya kimsingi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijidhihirisha kwenye utamaduni wa China.

Tuzo mbalimbali zitatangazwa baada ya kuzingatia alama na tathimini ya mwisho kufanywa na waamuzi wa mashindano.

Majina ya washiriki 10 na nchi wanazotoka ambao walifika hatua ya fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya Maandishi ya Kichina Hanzi” kwa mwaka wa 2021 ni pamoja na:

1. Nath Deborshmi, Quality School International, India

2. Fajer Kseibi, Syria

3. Michael Mubaiwa – Chuo Kikuu cha Jiangsu, Zimbabwe

4. Tanishita Mari, Chuo cha Ufundi Stadi cha Teknolojia ya Mawasiliano, Japan

5. Passy Carles Riseph, Chuo Kikuu cha Shanxi, Jamhuri ya Kongo

6. Dana Dyussembayeva, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Huazhong Cha China, Kazakhstani

7. Jacob Steele Ellis, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Qinghai, Marekani.

8. Guillermo Puig, Chuo Kikuu cha Lugha za kigeni cha Xi’an, Argentina

9. Richard Michel Thomas Gordon-Martins, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Chengdu, Ufaransa

10. Christoph Stahl, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing, Ujerumani. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha